Monday 1 December 2014

RAIS KIKWETE KUWASHUGHULIKIA WATUHUMIWA SAKATA LA ESCROW


BUNGE limeazimia kuwajibishwa kwa mawaziri Profesa Sospeter Muhongo, Profesa Anna Tibaijuka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema, kutokana na sakata la uchotaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu (BoT) kwa kutaka mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi wao.Mbali na hao, yumo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).    
   
Aidha, Waziri Mkuu Mizengo Pinda ameahidi kuwa Serikali itatekeleza maazimio yote manane yaliyopitishwa jana jioni na Bunge baada ya mjadala mkali wa siku tatu na mvutano wa siku moja juzi katika kupitisha maamuzi hayo ambayo yalifikiwa kwa maridhiano.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe alisoma maazimio hayo manane jana bungeni baada ya kufikiwa kwa maridhiano kati ya Kamati yake, Kambi ya Upinzani, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali.

Maazimio
Katika azimio la pili, Zitto alisema viongozi hao wa umma na maofisa wa ngazi za juu serikali wanapaswa kuwajibika kwa sababu wamehusishwa na vitendo vya kijinai katika sakata hilo, linalohusisha kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania (IPTL).
“Kwa kuwa vitendo vya kijinai wanavyohusishwa navyo viongozi wa umma na maofisa wa ngazi za juu serikalini, vinakiuka pia maadili ya viongozi wa umma kuwanyima viongozi na maofisa hao uhalali wa kuendelea kushikilia nafasi za mamlaka katika uongozi wa umma;
“Hivyo, basi Bunge linaazimia kwamba Waziri wa Nishati na Madini,  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco wawajibishwe, kwa kuishauri mamlaka ya uteuzi wao kutengua uteuzi wao,” alisema Zitto.
PAC katika mapendekezo yake bungeni, ilitaka Muhongo, Maswi, Jaji Werema, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele na Waziri Mkuu Pinda wawajibike kutokana na sakata hilo, lakini wabunge wengi walisema Masele na Waziri Mkuu Pinda hawakuhusika katika sakata hilo.
Aidha, kwa mujibu wa Zitto, Bunge limeazimia kuwa Taasisi ya Kupambana  na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Jeshi la Polisi na vyombo vingine husika vya ulinzi na usalama, vichukue hatua
stahiki kwa mujibu wa sheria  za nchi kwa watu wote waliotajwa kuhusika na vitendo vyote vya jinai, kuhusu miamala ya akaunti ya Tegeta Escrow, na watu wengine watakaogundulika baada ya uchunguzi mbalimbali unaondelea katika vitendo hivyo vya jinai.
Miongoni mwao ni mmiliki wa kampuni ya PAP, Harbinder Singh Sethi, James Rugemalira wa VIP Engineering Ltd, Jaji Werema, Profesa Muhongo, Maswi, wajumbe wa Bodi ya Tanesco, ambao inasemwa kuwa walihusika kwa namna moja au nyingine kufanikisha kufanyika kwa miamala haramu ya fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow kwenda PAP na VIP Engineering and Marketing Ltd.
*Wabunge
Azimio jingine la Bunge ni kuazimia Kamati za Kudumu za Bunge
kuwawajibisha viongozi wake kwa kuwavua nyadhifa zao kutokana na kushiriki kwa namna moja au nyingine katika sakata hilo.
Hao ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bajeti Andrew Chenge, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco.
Chenge na Ngeleja wametajwa kunufaika na fedha za mwanahisa Rugemalira kwa Chenge kupewa Sh bilioni 1.6 na Ngeleja Sh milioni 40.2, kwa mujibu wa taarifa ya CAG na PAC.
“Hivyo basi, Bunge linaazimia kwamba Kamati husika za Kudumu za Bunge zichukue hatua za haraka na kwa vyovyote vile kabla ya Mkutano wa Kumi na Nane wa Bunge, kuwavua nyadhifa zao wenyeviti tajwa wa Kamati husika za Kudumu za Bunge,” alisema  Zitto.
*Majaji
Kuhusu ushiriki wa majaji katika kashfa hiyo, alisema Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, imeweka utaratibu mahsusi wa kushughulikia nidhamu ya majaji, ambao kwa mujibu wa Katiba hiyo, unamtaka Rais aunde Tume ya Uchunguzi ya Kijaji kuchunguza tuhuma za u

No comments: