kurudi nyumbani kuleta zawadi alizonyakuwa hivi karibuni ,msanii huyu nguli wa Bongo fleva leo ameshapaa kwenda kwa Obama na Leo anatarajia kufanya shoo moja ya hatari sana kwa ajili ya Uhuru wa Tanzania...Cheki matangazo ya shoo atakazofanya hapa chini.....
Saturday, 6 December 2014
DIAMOND AHAMIA MAREKANI
kurudi nyumbani kuleta zawadi alizonyakuwa hivi karibuni ,msanii huyu nguli wa Bongo fleva leo ameshapaa kwenda kwa Obama na Leo anatarajia kufanya shoo moja ya hatari sana kwa ajili ya Uhuru wa Tanzania...Cheki matangazo ya shoo atakazofanya hapa chini.....
GAIDI ALIYELIPUA MABOMU ARUSHA AFARIKI AKIWA HOSPITALI.
Hatimaye Abdulkarimu Thabiti Hasia aliyekuwa akituhumiwa kwa ugaidi, amefariki katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru alipokuwa amelazwa kwa miezi sita akiwa mikononi wa polisi.
JINSI UKIMWI ULIVYOANZA AFRIKA
Ulianzia Jamhuri ya Demkorasia ya Congo (DRC) na vitendo vya ngono kwenye vituo na safari za treni mjini Kinshasa vilichochea ugonjwa huo kuanza kuenea kwa kasi hadi nje ya mipaka ya nchi hiyo.
JELA KWELI KUBAYA...KENYATTA AFURAHIA KUACHIWA HURU
RAIS Uhuru Kenyatta ameelezea kufurahishwa na uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC), kutupilia mbali kesi ya jinai iliyokuwa ikimkabili, baada ya Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama hiyo, Fatou Bensouda kuondoa mashitaka dhidi ya Rais huyo.
MMAREKANI MWEUSI MWINGINE APIGWA RISASI..
Mmarekani mwingine mweusi ambaye hakuwa na silaha ya aina yoyote ameuawa kwa kupigwa risasi na polisi mzungu huku maelfu ya Wamarekani wakiendelea kufanya maandamano kupinga mauaji ya kibaguzi yanayowalenga Wamarekani wenye asili ya Afrika.
Friday, 5 December 2014
ZITTO KABWE KURUDI CHADEMA ATOA SHARTI MOJA TU...
Harufu ya kuisha kwa mgogoro baina ya Zitto Kabwe na chama chake cha Chadema inanukia, lakini mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini anataka kuwapo na mazungumzo kubaini tatizo ili atakayebainika kuwa alifanya makosa awe tayari kuomba radhi hadharani.
MAMA WA KAMBO ALIYEMCHINJA MTOTO HUKO MARA NAE ACHINJWA.....
Tukio lilitokea hivi karibuni mkoani Mara la mama wa kambo kumchinja mtoto wake kwa kutumia panga hadi kufariki, limechukua sura mpya baada ya mama huyo nae kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali kwa kukatwa katwa na mapanga mpaka kufariki.
Tukio la kukatwa katwa mapanga mama huyo limetokea baada ya wananchi wa kijijini hapo walioshikwa na jazba kali kwa kutokubaliana na kitendo cha kinyama alichomfanyia mtoto huyo kwa kumkatishia maisha yake.
MTOTO WA AJABU AZALIWA DODOMA MADAKTARI NA WAUGUZI WAPIGWA NA BUTWAA
BINTI AOLEWA KWA KILO MBILI TU ZA SUKARI
Mmoja wa wanafunzi walioongoza mtihani wa Taifa wa Darasa la saba mwaka huu mwenye umri wa miaka 16 anadaiwa kuozwa kwa mwanaume mwenye miaka 50 baada ya wazazi wake kupewa sukari kilo mbili kama mahari.Kutokana na hali hiyo mtandao wa kuelimisha jamii kuhusu ukeketeji Mkoani Kilimanjaro NAFGEM umefanya jitihada za kumuokoa pamoja na wanafunzi wengine15 waliotaka kufanyiwa vitendo vya ukeketaji kwa ngariba.
Thursday, 4 December 2014
‘Mrwanda chaguo langu’
Dar es Salaam. Kocha mkuu wa Simba, Patrick Phiri amemrudisha kundini mshambuliaji Danny Mrwanda akieleza kuwa ndiye alikuwa chaguo lake.
Tayari, Mrwanda amepewa na uongozi wa klabu hiyo mkataba wa miezi sita huku kocha huyo Mzambia akiwa hana mpango na kiungo mshambuliaji raia wa Gambia, Omary Mboom.
Phiri alieleza jana kuwa roho yake imesuuzika baada ya Mrwanda kupewa mkataba wa miezi sita wa kuichezea Simba.
Jumatatu iliyopita, Mrwanda alisaini kuichezea timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi huku Phiri akisikitika kumkosa mshambuliaji mwingine wa zamani wa klabu hiyo, Mussa Hassan ‘Mgosi’ aliyeko Mtibwa Sugar.
Phiri aliliambia gazeti hili jana kuwa anamfahamu Mrwanda kwa muda mrefu, yeye ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa, amefurahi kumpata, atamsaidia kwenye safu ya ushambuliaji.
BAADA YA DIAMOND KUTWAA TUZO 3 CHANNEL O PRODUCER WAKE AANZA KUTOA MALALAMIKO
MGOGORO WA MPAKA KATI YA TANZANIA NA MALAWI..HALI BADO NI TETE
Kile kilichoonekana kuanza kama mzaha kati ya Tanzania na Malawi kuhusu umiliki wa Ziwa Nyasa, sasa kimeanza kuchukua sura mpya kwa kila nchi kuendelea kutekeleza kitu inachokiamini kuwa ni sahihi.
KOREA KASKAZINI YAISHUTUMU MAREKANI KWA KUTENGENENZA NA KUSAMBAZA VIRUSI VYA EBOLA BARANI AFRIKA
Koreas Kaskazini imeishutumu Marekani kwa kusambaza makusudi virusi vya ugonjwa wa Ebola na kwamba inatengeneza silaha hiyo ya kibailojia ili kuwa taifa lenye nguvu zaidi duniani.
LHRC YASIKITISHWA NA KAULI YA PINDA KUWA HANA UHAKIKA FEDHA ZA ESCROW NI ZA NANI..
Kituo cha sheria na haki za binadamu kimesema kimesikitishwa na kauli aliyoitoa waziri mkuu Mh Mizengo Pinda bungeni wakati akiahirisha bunge kuwa hakuna uhakika kwamba fedha zilizokuwa katika akaunt ya Escrow kama ni za serikali ama la jambo ambalo amesema kwa kufanya hivyo ni kutaka kuwalinda waliohuska katika wizi huo.
UKAWA WAANZA KUSALITIANA ARUSHA
VYAMA vinne vya upinzani vilivyoungana na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vimeshindwa kuachiana nafasi za uongozi mkoani Arusha, katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba 14.
Mh.ZITTO KABWE APATA MCHUMBA
MBUNGE Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Zuberi Kabwe amemtambulisha mchumba wake mpya anayetarajia kufunga nae pingu za maisha hivi karibuni.
188 WAHUKUMIWA KIFO NCHINI MISRI
Mahakama moja ya Misri imewahukumu kifo wafuasi 188 wa harakati ya Ikhwanul Muslimin kwa madai ya kuhusika kwenye shambulio lililotokea mwaka 2013 katika kituo cha polisi mjini Cairo. Hukumu hiyo ilitangazwa hapo jana ambapo watu hao wanadaiwa kushambulia na kuua askari kadhaa wa usalama. Wakati huo huo maelfu ya wananchi wa Misri wameandamana nchini humo kupinga uamuzi wa mahakama wa kumfutia mashtaka yote yaliyokuwa yanamkabili dikteta wa zamani wa nchi nchi hiyo Hosni Mubarak.
Waandamanaji hao huku wakitoa nara za kupinga serikali na kulaani utawala wa kijeshi wa Misri, wamesema kuwa hawatosalimu amri hadi pale matakwa yao yatakapotekelezwa. Polisi ya Misri imefunga barabara zote zinazoelekea katika Meidani maarufu ya mjini Cairo ambako hukusanyika waandamanaji, baada ya kuanza wimbi jipya la malalamiko ya wananchi ya kupinga kufutiwa mashtaka Hosni Mubarak.
SIRI YA MTUNGI SEASON 2 HIYOOOOOOOOO KUANZATAREHE 7 NDANI YA TBC1..
Akizungumza jijini jana, Mtayarishaji wa tamthilia hiyo, Louise Kamin kutoka Shirika Lisilo la Kiserikali la Media for Development International Tanzania (MFDI-TZ) alisema kuwa sehemu ya pili ya tamthilia hii inakamilisha Siri ya Mtungi kufuatia msisimko mkubwa wa msimu wa kwanza.
AFCON 2015: MAKUNDI YATAJWA
Upangaji wa makundi ya timu kumi na sita zilizofuzu kucheza fainali za mashindano ya 30 ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2015 yamefanyika katika mji mkuu wa Equatorial Guinea, Malabo.
Wednesday, 3 December 2014
SPIKA: MSIOE WANAWAKE WALIOKEKETWA...
Spika wa Bunge la Uganda Bi Rebecca Kadaga amewashauri wanaume kutowaoa wanawake waliokeketwa akiwataja kuwa mzigo ambao hauwezi kuijenga jamii.
VINARA MAUAJI YA WANAWAKE DAR,WAKAMATWA
Zaidi ya Wanawake 11 wameuawa Dar es Salaam katika kipindi cha miaka miwili na kutupwa barabarani au mitaroni huku miili yao ikiwa imefanyiwa vitendo vya unyama na udhalilishaji.
WABADILISHANA WAKE ZAO BAADA YA KUFUMANIANA
Tuesday, 2 December 2014
VIRUSI VYA UKIMWI VYAPUNGUA NGUVU......
Utafiti mkubwa wa kisayansi umeonyesha kuwa virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi vya HIV, vinapungua makali yake na kushuka kwa uwezo wake wa maambukizi kwa jinsi vinavyobadilika. Watafiti katika chuo kikuu cha Oxford nchini Uingereza wamefanya ugunduzi huo walipowafanyia uchunguzi mamia ya wanawake nchini Botswana.
Monday, 1 December 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)