Saturday, 13 December 2014
ROSE MUHANDO APEWA MIMBA NA MCHEZA SHOO WAKE...
Haya ni madai mazito! Mwimbaji nyota wa muziki wa Injili Bongo, Rose Muhando, anadaiwa kutundikwa mimba a.k.a ujauzito unaomfanya hivi sasa kutumia muda mwingi kujificha ndani....
Friday, 12 December 2014
VX LACHOMWA MOTO NA WANANCHI BAADA YA KUGONGA NA KUUA MADEREVA 3 WA BODABODA
Gari aina ya Toyota VX likiwaka moto baada ya kuchomwa na wananchi mchana leo Bunju B jijini Dar kwa kusababisha ajali na kuuwa madereva watatu wa bodaboda.
JOKATE NA MILLARD AYO NI WAPENZI???????????
Kutana na mwanadada ambaye anaendesha maisha yake kwa kazi mbalimbali zikiwemo uigizaji, muziki, uanamitindo, ujasiriamali na utangazaji.
YANGA YAMTEMA KHAMIS KIIZA
Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika , klabu ya Yanga ipo mbioni kukatisha mkataba na mshambuliaji Hamis Kiiza raia wa Uganda,
WEMA ATISHIA KUMPA KICHAPO PENNY,KISA TABIA YA UMBEA.....
Thursday, 11 December 2014
ITS NOW OFFICIAL; MENGI AMVISHA PETE YA UCHUMBA K-LYN WAKIWA DUBAI...
Tajiri anayeshika nafasi ya pili hapa Tanzania Mh Reginald Mengi amemchumbia aliewahi kuwa Miss Tanzania 2001 Jacqueline Ntuyabaliwe (Klyn)
Dk.REGINALD MENGI AAMUA KUTANGAZA TAARIFA YA HABARI MWENYEWE KISA UHABA WA WATANGAZAJI WASOMI...
MISS TANZANIA ATINGA TOP TEN ZA MISS WORLD 2014...SOMA NAMNA YA KUMPIGIA KURA
FINAL YA MISS WORLD 2014 NI 14-12-2014 SIKU ZIMEBAKI CHACHE TUMPIGIE KURA MISS TZ 2013
KUPIGA KURA NI RAHISI
NENDA PLAY STORE DOWNLOAD APPLICATION INAITWA MISS WORLD ZIPO NYINGI LAKINI CHAGUA ILIYOANDIKWA MISS WORLD LIMITED
UKISHA DOWNLOAD UTAONA PA KUCHAGUA LUGHA, CHAGUA KIBENDERA KILE CHA ENGLAND
ITATOKEA PICHA MOJA YA MSHIRIKI YEYOTE CHINI YAKE PAMEANDIKWA VIEW CONTESTANTS BONYEZA HAPO ILI UMTAFUTE HAPINESS WATIMANYWA
YATATOKEA MAJINA YA NCHI NA PICHA ZA WASHIRIKI NCHI ZIMEPANGWA KWA HERUFU SO WEWE TAFUTA "T"
UTAIONA TANZANIA NA PICHA YA HAPINESS CLICK KATIKA HIYO PICHA AU JINA TANZANIA. ITATOKEA PICHA KUBWA YA HAPPY KWA CHINI BONYEZA ADD TO TOP 3...ITASEMA CONTESTANT ADDED! RUDI MWANZO ONGEZA WASHIRIKI WENGINE WAWILI WA NCHI NYINGINE ILI UWEZE KUPIGA KURA
FANYA UZALENDO KWA KUSHARE POST HII
RAIS KIKWETE AMTUNUKU NISHANI MUUZA CHIPSI WA BUGURUNI
"Hongera kwa ushupavu uliouonyesha...", Rais Jakaya Mrisho Kikwete anaonekana kumwambia kijana Kassim Saidi Kassim wakati wa kupiga picha ya pamoja, baada ya kumtunuku Nishani ya Ushupavu Ikulu jijini Dar es salaam. Wengine katika picha ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda.
WALIOTEKWA NA KUSULUBIWA NYUMBANI KWA WEMA SEPETU HAWA HAPA
JAMAA wawili, mmoja fundi umeme, Rashid Balazi na Juma Bushiri wanadaiwa kunusurika kifo baada ya kutekwa na kusulubiwa nyumbani kwa msanii wa sinema za Kibongo, Wema Sepetu (pichani) wakituhumiwa kukwapua simu ya bei mbaya ya mpambe wa mwanadada huyo, Petit Man, Amani limeichimba kwa kina.
RC MWANZA: MARUFUKU KUWAPIGA WAMACHINGA MABOMU YA MACHOZI
Mkuu Mpya wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amelitaka jeshi la polisi mkoani Mwanza kutotumia nguvu pamoja na kufurumusha mabomu ya machozi kuwatimua wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama machinga mara wanapoombwa na halmashauri ya jiji bila kupata maelekezo.
NI NOUUUUMA....DAVIDO AMPA DONGO LA NGUVU DIAMOND...NOUUMA SANA
Huhitaji kujifikiria mara mbili kuamini kuwa Davido na Diamond haziivi tena kwa sasa!
Yote yalianza baada ya Davido kutweet ‘N they cheat again, Lol’ baada ya Idris kutangazwa mshindi wa Big Brother Hotshots. Tweet hiyo ikimfanya Davido atukanwe matusi ya kila aina kutoka kwa Watanzania.
HUYU NDIYE MSANII WA BONGO MOVIE MWENYE WATOTO WENGI KULIKO WOTE.....ANA WATOTO 8...
MWONGOZAJI na mwigizaji mahiri katika tasnia ya filamu za Bongo, Kulwa Kikumba ‘Dude’, ametaja idadi ya watoto wake akisema wapo wanane tu. Amekanusha vikali kuwa na timu ya mpira (watoto 11) idadi inayovumishwa na wengi.
Dude anatajwa kuwa ni msanii anayeongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto kwa wasanii wengine wa kiume wa Tanzania.
Wednesday, 10 December 2014
WOLPER AACHANA NA MAMBO YA ANASA AWAKUMBUKA WAZEE....
Staa wa filamu Bongo Jacqueline Wolper Massawe akisalimiana na Sista wa Kanisa Katoliki la Msimbazi, jijini Dar.
STAA Jacqueline Wolper Massawe, ambaye ni muigizaji mahiri wa filamu, amewapiku nyota wenzake wa tasnia hiyo baada ya kufanya kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa Jumamosi iliyopita kwa namna tofauti kabisa, kwani badala ya kuita marafiki kwenye pati kubwa inayoambatana na vyakula na vinywaji, yeye alikwenda kuwatembelea wazee wanaolelewa katika Kanisa Katoliki la Msimbazi, jijini Dar.
KIMENUKA TENA HUKO KILOSA,BARABARA DAR-DOM YAFUNGWA MASAA MAWILI
WATU kadhaa wamejeruhiwa katika vurugu zilizotokea jioni ya jana huko Dumila mkoani Morogoro kati ya wakulima na wafugaji ambapo polisi wameingilia kati na kutumia mabaomu ya machozi kutuliza ghasia hizo.
MATOKEO UEFA HAYA HAPA....
Michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya imeendelea usiku wa jana ikiwa kwenye mzunguko wake wa mwisho wa hatua ya makundi . Katika michezo iliyopigwa jana timu ya Arsenal toka England ilifanikiwa kushinda kwenye mchezo wake dhidi ya Galatasaray ya Uturuki kwa matokeo ya 2-4 katika mchezo uliopigwa huko Istanbul.
Tuesday, 9 December 2014
WALE MAPACHA WALIOUNGANA HUKO INDIA WAPATA MPENZI..
Mapacha ambao wameungana huko Bengal Magharibi Ganga na Jamuna Mondal 45, wamesema hawajawahi kuwa na mpenzi katika maisha yao kwa sababu ya kukataliwa kutokana na mwonekano wao.
Mabinti hao ambao wanatumia mikono minne na miguu mitatu wamesema kwa sasa wanafuraha ambayo hawajawahi kuwa nayo katika maisha yao baada ya kukutana na mwanaume aliyewapenda kwa mara ya kwanza Mwalimu Jasimuddin Ahmad.
ALIYEZAMISHWA SULULU KICHWANI APONA KABISA.....
HAKUNA neno jingine la kutumia zaidi ya kusema; KWELI MUNGU MKUBWA! Ni miezi mitano sasa imekatika tangu kusambaa kwa picha mitandaoni zilizomwonesha mwanaume mmoja akiwa ameshindiliwa sululu kichwani hukukisa kikiwa hakijulikani.
INASIKITISHA NA INAUMA SANA..BABA WA KAMBO AMNYONGA MTOTO KISA WIVU WA MAPENZI.......
Abdulrahman Hamis Clemensi enzi za uhai wake.JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia Zamili Shabani kwa madai ya kumnyonga hadi kumuua mtoto wake wa kambo, (mwaka mmoja na nusu) huku mauaji hayo yakihusishwa na wivu wa mapenzi.
HOUSEGIRL ANUSURIKA KIFO
Msaidizi wa kazi za ndani (hausigeli), Rehema Ally (17), mkazi wa Yombo, Machimbo Mwisho, Ilala jijini Dar, amechanwachanwa kwa wembe na kisu sehemu mbalimbali za mwili wake, hali iliyosababisha alazwe katika Hospitali ya Amana kwa matibabu.
MAUAJI YAENDELEA JIJINI MBEYA
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA NTOKELA WILAYANI RUNGWE ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA CHESCO MAHENGE (41) ALIKUTWA AKIWA AMEUAWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI NA WATU WASIOFAHAMIKA.MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA KANDO YA BARABARA KWENYE MASHAMBA YA CHAI MNAMO TAREHE 07.12.2014 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAPINDUZI, KIJIJI CHA NTOKELA, KATA YA ISONGOLE, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA.
POLISI AMTETEA MTUHUMIWA MAHAKAMANI KISUTU
KESI ya kughushi inayomkabili mfanyabiashara, Hans Aingaya Macha imechukua sura mpya, baada ya askari Johanes Mgendi mwenye namba E 2982 kutoa ushahidi katika upande wa mtuhumiwa kwenye kesi hiyo.
SNURA ATUMIA SIMU KUTAPELI
MSANII wa filamu na muziki Bongo, Snura Mushi (pichani) amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutumika kwa utapeli kupitia namba yake ya simu.
BAADA YA DAVIDO KUTOA KAULI CHAFU DHIDI YA WATANZANIA, DIAMOND NAE AFUNGUKA..
Baada ya idris kushinda ule mshiko katika mashindano ya BBA kule kwamadiba davido akatoa kauli kwamba ‘they cheat again’ kwaupande wake Diamond ilimuuma sana hiyo kauli na kuhisi kwamba hata kwenye tuzo za Channel O pia inaonekana walicheat pia..
Monday, 8 December 2014
IDRIS KIDUMEEEEEEE ALAMBA DOLALI LAKI TATUUUUUUU ZA BIG BROTHER AFRICA HOTSHOTS..
Idris Sultan ndio mshindi wa Big Brother Africa Hotshots. Baada ya kutupa karata yake kwa takriban miezi miwili ndani ya jumba hilo lililopo nchini Afrika Kusini, Afrika imemchagua kuwa mshindi wa msimu huu wa Big Brother na hivyo kushinda kitita cha $300,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 514 za Tanzania.
CRISTIANO RONALDO AVUNJA REKODI YA HAT TRICKTRICK LA LIGA
Kocha wa Real Madrid, Muitaliano Carlo Ancelotti ameelezea uwepo wa Cristiano Ronaldo’s katika kikosi chake kama faida baada ya nyota huyo kufunga goli tatu peke yake (Hat-trick) na kufikisha jumla ya goli 200 katika kigi hiyo wakati madrid ilipoishindilia Celta Vigo 3-0.Katika pambano hilo, nyota huyo toka ureno, Cristiano Ronaldo alifunga goli zote tatu na hivyo kuvunja rekod ya hattrick ya la liga akifikisha 23, moja zaidi ya Magwiji Alfred Di Stefano na Telmo Zarra, huku zikiwa tatu zaidi ya mpinzani wake wa karibu Lionel Messi mwenye 20. Ikumbukwe nyota huyo sasa amefikisha jumla ya goli 200 katika michezo 178 pekee ya La Liga aliyoshiriki ikiwa ni kasi zaidi ya nyota yeyote.
Sunday, 7 December 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)