Friday, 21 November 2014

GHASIA ZAZUKA BUNGE LA NIGERIA


Ghasia zimezuka katika Bunge la taifa nchini Nigeria alhamisi baada ya maafisa wa usalama kujaribu kumzuiya spika wa Bunge la wawakilishi kuingia katika eneo la Bunge.

Polisi imeiambia Sauti ya Amerika kwamba ilifyatua gesi ya machozi wakati wa ghasia hizo baina ya majeshi ya  usalama na takriban wafuasi 200 wa spika Aminu Tambuwal.

Tambuwal  alikikasirisha  chama tawala  cha People’s Democratic Party baada ya hivi karibuni kuhamia chama cha upinzani cha All Progressive Congress.

Magazeti ya Nigeria yanaripoti kuwa dazani ya maafisa wa idara ya usalama ya Nigeria walichukua udhibiti wa Bunge kabla ya kikao cha Alhamisi ambacho Tambuwal alitakiwa kukiendesha.

Taarifa zinasema spika alizuiwa kuingia ndani  lakini Wabunge wengine waliingilia  kati, wakaharibu mlango mkuu na kumuingiza Tambuwal ndani ya eneo hilo.

No comments: