Thursday 4 December 2014

UKAWA WAANZA KUSALITIANA ARUSHA


VYAMA vinne vya upinzani vilivyoungana na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vimeshindwa kuachiana nafasi za uongozi mkoani Arusha, katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Desemba 14.



Vyama vinavyounda Ukawa ni Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, lakini vyote vimesimamisha wagombea katika mitaa ndani ya mkoa wa Arusha, kinyume na makubaliano yaliyosainiwa na vion gozi wa kitaifa hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Kitendo hicho kimefanya CCM kutwaa kiulaini uongozi kwenye vijiji 183 kati ya 406.

Aidha chama hicho kimeshinda kwa rufaa katika mitaa sita kati ya 155 ambapo Mkoa mzima wa Arusha una vijiji 406 na mitaa 155. Chadema watetea.

Akizungumzia hali hiyo jana mjini hapa, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema makubaliano ya viongozi wa juu ya Ukawa ya kuweka mgombea anayekubalika iko pale pale.

Alikiri vyama vinavyounda Ukawa kusimamisha wagombea kila kimoja kivyake mkoani Arusha, lakini akasisitiza kuwa, hiyo haina maana kwamba makubaliano yao ya kushirikiana yamevunjwa.

Alisema wamefanya hivyo kwa sababu maalumu ambayo wao wanaijua, lakini umoja wao uko pale pale na makubaliano yanaheshimika kwa asilimia kubwa.

Mwenyekiti huyo aliwataka wanachama wa Ukawa kutokuwa na wasiwasi, kwani wamefanya hivyo kwa kuangalia ni namna gani watashirikiana katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

CCM yatamba

Akizungumza na gazeti hili jana ofisini kwake, Katibu wa CCM mkoa wa Arusha, Alphonce Kinamhala alisema ushindi huo unatokana na utekelezaji mzuri wa ilani ya chama ambayo imekuna wananchi wengi mkoani humo.

Alisema kwa sasa CCM ina kazi ndogo ya kupambana na vijiji 378 vilivyosalia na kwamba hali inakwenda vizuri na wana uhakika wa kushinda katika vijiji vilivyosalia katika uchaguzi huo wa Desemba 14, mwaka huu.

Katibu huyo alisema mbali ya ushindi wa vijiji hivyo, pia CCM imeshinda vitongoji 688 sawa na asilimia 46 kati ya vitongoji 1,483 na kilichobakiwa ni kushindana katika vitongoji 795 pekee.

Alisema baada ya kuzindua kampeni zake mwishoni mwa wiki iliyopita, hali inaendelea vizuri na hakuna malalamiko ya kuwapo vurugu kwenye mikutano ya kampeni wilaya zote.

Kinamhala amevitaka vyama vya upinzani kufanya kampeni za kistaarabu zitakazotoa nafasi kwa wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura.

Alisema wajibu wa kupiga kura ni haki ya msingi ya kila mtanzania mwenye sifa na endapo kampeni zitakuwa na vurugu, wengi watashindwa kujitokeza kupiga kura siku hiyo.

“Naomba kutoa mwito kuwa ni jukumu letu sote kufanya kampeni za kistaarabu na sera nzuri zenye ujumbe kwa wananchi ambazo zitawahamashisha wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowaona wanafaa kuwaongoza,’’ alisema.

Wakati hayo yakijiri mkoani Arusha, hali hiyo imejitokeza pia mkoani Morogoro katika Kata ya Chamwino, ambako iliripotiwa katika baadhi ya vyombo vya habari kwamba CUF imesimamisha wagombea katika mitaa yote 15 baada ya kushindwa kuafikiana kuachiana mitaa na Chadema.

Ilidaiwa na CUF kwamba viongozi wa Chadema walishindwa kuwaachia mitaa mitano, ambayo CUF ina nguvu na kukubalika na wananchi.

Ilielezwa kwamba Chadema ilishauriwa kuchukua mitaa 10, lakini ikashindwa kuheshimu makubaliano kwa kusimamisha wagombea mitaa yote.

Mmoja wa viongozi wa CUF Kata ya Chamwino, Omari Mwansenga, alikaririwa akisema,“wenzetu wa Chadema wameshindwa kuheshimu makubaliano ya kuachiana mitaa, CUF ina mitaa mitano yenye wafuasi na kukubalika na itasimamisha wagombea.”

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa CUF, Wilaya ya Morogoro Mjini, Abdallah Mambo, alikiri kuwapo migongano hiyo katika umoja huo ingawa alisema suala hilo liko chini ya maelekezo ya viongozi wa vyama washirika ngazi ya wilaya.

Makubaliano

Kutoafikiana kwa vyama hivyo, kunakwenda kinyume na makubaliano yaliyosainiwa na viongozi wakuu wa vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD vinavyounda Ukawa.

Novemba 4 mwaka huu, vyama vya siasa vinavyounda Ukawa vilisaini mwongozo wa ushirikiano katika uchaguzi wa se

No comments: