Saturday, 27 December 2014
HUU NI UNYAMA..BUBU ABAKWA NA WANAUME WATANO
MKAZI wa kitongoji cha Chingale, kijiji cha Mtakuja kata ya Temeke katika Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara ambaye ni bubu, Asumini Fakihi amebakwa na watu watano wasiojulikana na kumsababishia majeraha na kulazwa katika Hospitali ya Mkomaindo mjini Masasi.
WAKAMATWA KWA KUIBA SANAMU YA BIKIRA MARIA...
Vijana watatu Songea wametakiwa kwenda na wazazi wao kutubu dhambi za kutaka kuiba sanamu la Bikira Maria katika Kanisa Katoliki la Kigango cha Samora.
PATCHO MWAMBA AKANUSHA KUFUMANIWA...
Mwigizaji na mwanamuziki wa Bendi ya FM Academia, Patcho Mwamba amekanusha vikali taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa amefumaniwa akiwa na mke wa mtu na kupokea kipigo.
TAARIFA KAMILI YA BOMU LILILOLIPUKA HUKO RUVUMA NA KUMUUA MLIPUAJI
Kamanda wa polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela akitoa maelezo kwa DCP Diwani Athumani ambaye aliwasili mkoani humo jana kwaajiri ya bomu la kutengenezwa kienyeji ambalo askari wa doria walinusurika kurushiwa na kumlipukia mlipuaji wa bomu hilo ambaye
alifariki papo hapo.
Askari WP Mariam mwenye namba 8616 akiwa amelazwa wodi ya majeruhi hospitali ya Mkoa baada ya kujeruhiwa mkono wa kushoto kwenye bega baada ya vipande vya bomu kumfikia akiwa na askari wenzake kwenye doria siku ya sikukuu ya krisimas.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiuangalia mwili wa mtuhumiwa wa ulipuaji wa bomu ambaye alitaka kuwarushua askari wa doria wakati wa sikukuu ya krismas kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. (PICHA NA AMON MTEGA ,SONGEA.
.....................................................
MMTALAKA WA MBUNGE AWASHANGAA WANAOMWITA MBURULA...
Mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya mjini Mh.Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’, Faiza Ally.
Mzazi mwenzake na Mbunge wa Mbeya mjini Mh.Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’, Faiza Ally amefunguka kuwa, watu wasidhani kuwa yeye ni mbulula kwa uamuzi wake wa kuvaa pempasi ukumbini bali aliamua tu.
MISS TANZANIA LOKAPU MIAKA 2 ILI KUREKEBISHA TABIA...
Tangu atangazwe aliyekuwa Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu mengi yameongelewa kuhusiana na tetesi za udanganyifu wa umri na vitu vingine kadhaa vinavyomhusu mrembo huyo ikiwemo suala la umri wake na kiwango cha elimu yake ambapo yeye mwenyewe alikanusha taarifa hizo.
DIAMOND:.."NIMEMPENDA ZARI ILI NIJULIKANE NCHINI UGANDA"..
Mapenzi bhana! Baada ya kutoka kimalavu na kumwagana na mwanadada mwenye mvuto Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kisha kuangukia kwenye ‘utamu’ wa penzi la mwanamama anayekimbiza Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameamua kuanika siri tano za kilichomvutia kwa staa huyo gumzo Afrika Mashariki.
HUYU NDIYE MTANGAZAJI MCHAFU ZAIDI ANAETANGAZA BBC
Raphael Tenthani
Katika maisha ya kawaida tumezoea kuona kuwa watangazaji na waandishi wa habari hupendelea kuonekana SMART kwani wao ni kioo cha jamii,,ila kwa hili ni tofauti....
Pichani ni Raphael Tenthani, mwakilishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) nchini Malawi.
Friday, 26 December 2014
Mh.MBUNGE AITELEKEZA FAMILIA BAADA YA NDOA KUVUNJIKA
Aliyekuwa mpenzi wake na mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi aka Sugu, Faiza Ally amemtupia lawama mzazi mwenzake kuwa hamjali mwanae baada ya kuachana.
Faiza alikuwa akiongea kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV ambapo alikiri kuwa kuachana na Sugu kunaendelea kumuumiza.
Wednesday, 24 December 2014
KAOLE SANAA GROUP LAFUFUKA TENA,LABATIZWA JINA JIPYAAAAAA....
Kundi kongwe la sanaa ya uigizaji na ngoma lililotoa vipaji vingi vya uigizaji hapa nchini, Kundi la Sanaa la Kaole “Kaole Sanaa Group” limerudi ila sasa kwa jina lingine..habari kamili ametueleza hapa, Halima Yahya “DAVINA”moja kati ya waliokuwa kaole na sasa wameasisi hii kaone, anasema;
BAADA YA KUENGULIWA UWAZIRI,TIBAIJUKA AHAMIA JIMBONI KWAKE....
Wananchi mkoani kagera wamepinga uamuzi wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete kwa kumuondoa madarakani waziri wa ardhi nyumba na makazi na kuwaweka kiporo viongozi wengine walioshiri kuhujumu pesa za akaunti ya Tegeta Escrow.
Wakiongea na ITV wananchi wa mkoa huo wamesema hawajajua nini hatima ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa tanzania Dk. kikwete kwa kuwaweka Kiporo mawaziri wengine waliohusika katika sakata hilo na kumuuondoa waziri Tibaijuka napia wamebaki na sintofahamu ambapo wamemtaka Rais kutoa ufafanuzi kuwa licha kumg’oa madarakani kiongozi huyo Je, Pesa hizo zitarudishwa kwenye akauti hiyo ya TEGETA ESCROW au la.
KUFUATIA SAKATA LA ESCROW KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI ASIMAMISHWA KAZI
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue, amemsimamisha kazi kwa muda Ndugu Eliakim Maswi (Pichani), Katibu Mkuu ya Wizara ya Nishati na Madini ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake, kama ilivyoelekezwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
BAADA YA KUPIGWA KIBUTI.....NICKI MINAJ ATOA VIGEZO VYA MWANAUME MPYA ANAEMTAKA.....
Baada ya kutengana na mpenzi wake safaree Samuels, Hitmaker wa nyimbo ya ‘Anaconda’ Nick Minaj ametaja vigezo vya mpenzi atakayekua naye kwa sasa aka BABY MPYA...
Monday, 22 December 2014
Mh ANNA TIBAIJUKA KUMGOMEA RAIS KIKWETE???????
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete amemaliza hutuba yake na Wazee wa Jiji la Dar es salaam na Kumalizia kwa Kumuwajibisha waziri wa Ardhi na Makazi, Anna Tibaijuka kwa kutengua wadhifa wake wa UWAZIRI.mh rais alisema "Waziri Tibaijuka alifanya makosa kimaadili; tumemwomba AnnaTibaijuka apumzike tumteue mwingine!"
Pia Mh Rais amesema kuwa "Waziri wa Nishati na Madini Prof. Muhongo huyu nimemuweka kwanza kiporo maana bado uchunguzi unafanyika"...
Sunday, 21 December 2014
PLUIJM AWAAHIDI WANA YANGA SOKA LA KUVUTIA NA LA KUSHAMBULIA
Kocha mpya wa Yanga Hans Pluijm leo amefanya mkutano wa kwanza na waandishi wa habari tangu apewe mikoba ya kuifundisha tena timu hiyo yenye maskani mitaa ya Kariakoo jijini Dar Es Salaam.
UTAFITI MZITO NA UCHAMBUZI WA STATUS ZA WHATSAPP HUU HAPA....
Habari za weekend wadau wangu....Najua wengi wenu mmejipumzisha na pia kuna mnaoendelea na kupiga mishemishe...Mungu awabariki..
Leo katika pita pita zangu nikakutana na utafiti huu ambao naamini sio wa kisayansi lakini ni muhimu kukushirikisha....Utafiti huu unahusu Status mbalimbali zinazopatikana kwenye profiles mbalimbali kwenye mtandao wa WHATSAPP...Bila kupoteza muda naomba tuungane kuzifuatilia status hizo na uchambuzi wake yakinifu:
"I luv u dady, can't wait to 've ur f" (Unakuta ni uzushi tu, hakuna chochote, hajaolewa wala nini, kama sio ufuska ni nn?)
AMTUPA MJUKUU WAKE DIRISHANI BASI LIKIWA KWENYE MWENDOKASI
Katika hali isiyo kuwa ya kawaida mama moja aliye kuwa akisafiri na mtoto wake mmoja na wajukuu zake wawili, aliamua kumtupa mjukuu wake wa miaka sita dirishani huku basi likiwa katika mwendo kasi na kusababisha kifo chake baada ya kufikishwa katika hospitali ya mkoa wa Singida.
HATA UWE PEDESHEEE KIASI GANI,KAMA HAUKO TAYARI KWA "MAMBO FLANI" HUWEZI KULA MZIGO KWA SHILOLE (SHISHI BABY)
Mwigizaji na mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Zuwena Mohamed, maarufu kama shilole amedai kuwa anaweza kufanya ujinga wowote humu duniani lakini linapokuja suala la mapenzi hapo yupo makini sana na kamwe hawezi kufanya ujinga wa kujisahau au kukurupuka tu kwa kumuangalia MTU alivyo kwa uzuri au pesa zake...
CR7 NOMA,AWEKA REKODI NYINGINE ULIMWENGU WA SOKA
Cristiano Ronaldo amekua mchezaji wa kwanza duniani kuzoa vikombe vyote kwa ngazi ya club vya ligi ya ndani ya nchi husika anayocheza akiwa na vilabu viwili tofauti akiwa na Man united Ronaldo alifanikwa kushinda mataji yafuatayo..
BAADA YA MTOTO WA RAIS OBAMA KUBEBA MIMBA,MAMA YAKE ASEMA MIMBA ZA MAPEMA NI KAWAIDA KWENYE FAMILIA YAO.....
Baada ya habari hii kusambazwa na kujadiliwa sana mitandaoni na kwenye vyombo mbalimbali vya habari..Mke wa Rais Obama,Michelle Obama alipokuwa kwenye mahojiano na kituo kimoja cha habari amefunguka bila kusita kuhusiana na ujauzito wa mwanae Malia Obama...Kufunguka huko kuliacha mshangao na wengine wakifurahia kile alichokiongea..Mama huyo bwana alitoa matamshi haya yafuatayo;
BAADA YA KUINGIA MKATABA WA BILIONI 8.5 NA WACHINA,DIAMOND AMPA ONYO JOKATE KIDOTI...
Baada ya mwanadada Jokate kupitia kampuni yake ya KIDOTI kuingia mkataba mnono wa bidhaa zake na kampuni ya wachina, msanii Dimaond Platnumz amefunguka haya yafuatayo…
LULU AFIKIRIA KUZAA, ASEMA KUZAA NI HESHIMA WALA SI KUZEEKA...
Mrembo na mwigizaji wa filamu hapa nchini, Elizabeth Michael “LULU” ameamua kufunguka na kusema mtazamo wake kuhusu swala la wasichana kuogopa/kukataa kuzaa kwakuofia kuwa watazeeka.
KITUKO; MKE AMKIMBIA MUMEWE KISA DOZI NZITO KITANDANI...
Hiki ni kituko cha mwaka kilichotukia katika kituo cha polisi bulenga, wakati mwanamke mmoja alipokuwa akiomba poo na huku akimtaka mumewe amsamehe na kumwachilia aende zake kutokana na mumewe kuwa na hamu ya kufanya ngono isiyo na koma. Ruth Nakyeyune,alikuwa akilia na hanyamazishwi kwa madhila apatayo kutoka kwa mumewe huku akimuomba mumewe mwenye asili ya Nigeria bwana Sultan Ali Baba..
MONALISA APINGA UAMUZI WA STEPS KUSHUSHA BEI ZA DVD ZA BONGO MOVIE,YADAIWA LENGO SI KUPAMBANA NA MAHARAMIA BALI NI KUZIUA KAMPUNI NYINGINE ZA KUSAMBAZA KAZI ZA WASANII ILI STEPS IBAKI PEKE YAKE
Yvonne Cherryl (Monalisa) mmoja wa waigizaji maarufu ambao wamepigana sana kuifikisha tasnia ya filamu Tanzania hapa ilipo leo ameonekana kutoridhishwa na hatua walioichukua kampuni ya Steps Entertainment kuuza filamu za kitanzania kwa shilingi 1500 badala ya 3000 kwa bei ya rejareja kuanzia mwakani mwezi wa pili.
Subscribe to:
Posts (Atom)