Sheddy amesema ameshangazwa baada ya kutoona jina lake likiandikwa kwenye video ya ‘Ntampata Wapi’.
“Biashara kweli ni matangazo na nilitakiwa niandikwe kweli kwenye ile video, lakini sasa kwa sababu imeshapita na vitu vingi vimeshatokea na ukiangalia kwenye video international wanafanya hivyo ila mpaka sasa hivi najaribu kujiuliza sijapata jibu kamili kwanini wanafanya hivyo,” Sheddy ameiambia E-News ya EATV.
“Ukiangalia video za West Africa za akina Davido, Wizkid wengi producer wa audio wanakuwa hawaandikwi kwenye video. Sasa sijui wanafuta ule mfumo wa wenzetu, sifahamu.”
No comments:
Post a Comment