Wednesday, 3 December 2014
HAPPY BIRTHDAY FAST JET......
Kampuni ya ndege ya fastjet, ambayo ni Kampuni yenye gharama nafuu kote Afrika, imeadhimisha miaka miwili ya kutoa usafiri wa anga barani Africa.
Fastjet ilianza biashara ya usafiri wa anga hapa Tanzania tarehe 29 Novemba 2012, ikifanya safari zake kutoka Dar es Salaam kwenda Kilimanjaro na Mwanza kupitia ndege yake aina ya A319.
Tangu wakati huo, Fastjet imepanua wigo wa mtandao wake nchini Tanzania pamoja na kuanzishwa kwa njia yake ya tatu kwenda Mbeya. Kwa sasa safari za Kimataifa za ndege hii ni pamoja na safari ya Dar es Salaam kwenda Johannesburg nchini Afrika ya Kusini, Lusaka nchini Zambia, Harare nchini Zimbabwe na Entebbe nchini Uganda.
Hadi sasa, ndege imeshasafirisha zaidi ya abiria 870,000 katika safari zake 8,200 ilizofanya zenye umbali wa takribani kilomita milioni 6.5 – ambapo utendaji wake kwa ujumla umevutia kwa asilimia 90 kwa mwaka 2014 kwa kuwa usafiri wenye uhakika na wa kuzingatia muda. Kampuni imejijengea kuwa ni ya uhakika, kuaminika na ya usafiri wenye gharama nafuu.
Nauli za Fastjet katika safari za ndani ya nchi hapa Tanzania zinaanzia dola za kimarekani 20 kwa safari moja, na nauli za kimataifa gharama ni ndogo kuanzia dola 50 kwa safari moja, zote ukiondoa kodi ya uwanja wa ndege na kodi ya serikali. Nauli hizi nafuu zimeifanya kampuni hii kutajwa kuwa ni yenye gharama nafuu kwa Afrika na ya tano kidunia kwenye unafuu wa bei ukilinganisha na makampuni mengine kupitia tovuti ya makampuni ya ndege, WhichAirline.com.
Fasjet inaamini unafuu wake wa bei unafanya safari za anga kupatikana kwa wingi kwa Waafrika wengi zaidi. Usemi huu ulihakikiwa kupitia utafiti uliofanywa na Fastjet muda mfupi baada ya uzinduzi wake, ambao ulionyesha kuwa asilimia 38 ya abiria wake walikuwa wanasafiri kwa mara yao ya kwanza ambapo kabla hawakuwa na uwezo wa kusafiri kwa anga.
“Usafiri wa anga wenye gharama nafuu ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi katika Afrika- hasa katika sekta ya biashara na utalii,” amesema Jimmy Kibati, ambaye ni Meneja mkuu wa kampuni ya Fastjet kwa Afrika Mashariki. “Hata kama kuna ndege zilizopo zinazounganisha majiji miwili, kwa kawaida ndege huwa inahusisha angalau kituo kimoja cha kusimama. Hivyo, nauli kubwa inayotozwa na mashirika ya ndege kwenye safari za njia hizi huwatenga wananchi wengi kufurahia urahisi na uokoaji muda unaotokana na faida ya kusafiri na ndege.”
Kulingana na Kibati, Fasjet imepiga hatua kubwa katika miaka hii miwili, licha ya changamoto ambazo kampuni imekuwa ikikabiliana nazo.
“Licha ya changamoto kubwa za udhibiti tulizokutana nazo wakati tunaanza upanuzi wa safari za kimataifa, serikali ya Tanzania imekuwa ikitutia moyo sana, kwa sababu hiyo tunawashukuru sana,” aliongeza Kibati. “Hii inatufanya tuwe na mtazamo chanya juu ya siku zijazo, pamoja na maoni yetu kwamba ukuaji wa uchumi katika Tanzania utaendelea, ukiendeshwa na tabaka la kati linaloibuka, na kuongezeka kwa viwango vya mapato ya hiari, ukuaji mkubwa katika ujasiriamali na uboreshwaji wa miundo mbinu ya uwekezaji.
Kibati pia alitoa maoni juu ya umuhimu wa kuwa na kitovu cha usafiri wa anga katika mji wa kibiashara wa Tanzania. “Dar es Salaam itaendelea kukua na kuwa kitovu cha viwanda na biashara katika Afrika na dunia kwa ujumla, hii inasababishwa na nafasi yake ya kuwa kama lango la Afrika Mashariki, maendeleo ya mafuta na akiba ya gesi na kuwa na miundo mbinu bora ya uwekezaji,”
Kuhusiana na usafiri wa anga kwa bei nafuu katika bara zima, Kibati alielezea, “Tunaamini kwamba kuna umuhimu mkubwa wa kuwa mfano wa ndege zenye gharama nafuu katika Afrika. Tumedhamiria kufanya kazi pamoja na serikali katika bara zima ili kukuza faida ya ushindani katika sekta ya anga. Hii itasababisha nauli ziwe nafuu kwa abiria. “
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment