Thursday, 4 December 2014
LHRC YASIKITISHWA NA KAULI YA PINDA KUWA HANA UHAKIKA FEDHA ZA ESCROW NI ZA NANI..
Kituo cha sheria na haki za binadamu kimesema kimesikitishwa na kauli aliyoitoa waziri mkuu Mh Mizengo Pinda bungeni wakati akiahirisha bunge kuwa hakuna uhakika kwamba fedha zilizokuwa katika akaunt ya Escrow kama ni za serikali ama la jambo ambalo amesema kwa kufanya hivyo ni kutaka kuwalinda waliohuska katika wizi huo.
Akizungumza katika makao makuu ya kituo hicho mkurugenzi wa utetezi na maboresho mwanasheria Harold Sungusia amesema kwa kauli aliyoitoa waziri mkuu bungeni kushangaza umma vile kamati ya bunge ya hesabu za serikali PAC imesema wazi kuwa fedha ni za umma.
Kwa upande wake afisa programu dawati la uangalizi wa serikali katika sakata la wizi wa fedha za umma Bw. Hussein Sengwa amesema miongoni mwa watu ambao wametajwa ndio walikuwa waandishi wa katiba mpya na ndiyo maana hata vipengele muhimu vya kuwabana viongozi wasiokuwa wadilifu walivifuta.
Aidha afisa programu dawati la bunge na uchaguzi Bw Hamis Mkindi amesema kutokana na sakata la IPTL watu wengi wameamka na kutaka kushiriki katika uchaguzi unaoendelea sasa wa viongozi wa serikali za mitaa ambao wameonekana kutaka kuwaweka viongozi wanaoona ni waadilifu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment