Thursday 4 December 2014

MFAHAM ZARI (The boss lady) KIUNDANI...




Jina lake halisi anajulikana kama Zarinah Hassan maarufu Zari. Alizaliwa Septemba 23, 1980 huko Jinja, Uganda, kati ya shule alizosoma ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jinja. Alikwenda Kampala na baadaye jijini London ambako alipata Diploma ya Cosmetology.Zari alianza kujishughulisha na masuala ya muziki akiwa shule ya msingi. Kwa kuungwa mkono na familia yake mwaka 2007, alirekodi wimbo wa kwanza Oliwange (Wewe ni Wangu), albamu hiyo ilimpa tuzo Channel O ikiwa video bora ya Afrika Mashariki. Tangu hapo alitoa vibao kadhaa. 


Mwanamuziki huyo ambaye ana asili ya India, Burundi, Uganda na Somalia, mwaka 2009 alipata tuzo ya mwanamuziki bora wa kike, huku mwaka 2008 akishinda tuzo ya Channel O akiwa mwanamuziki bora Afrika Mashariki. 

Usiyoyajua kuhusu Zari
Zarinah ni mwanamuziki anayeishi Afrika Kusini na mumewe Ivan Semwanga anayedaiwa kuwa ametengana naye kwa sasa. Ana watoto watatu aliozaa na mumewe huyo ambao ni Pinto, Didy na Quincy ambao nao pia wanaishi Afrika Kusini. Ni mjasiriamali na mfanyabishara maarufu na tajiri anayeuza zaidi vipodozi na nguo. Anamiliki magari ya bei ghali.
        

No comments: