Friday, 5 December 2014

MASHABIKI WA BARCELONA WAGOMEA JEZI MPYA


 
   


Nguvu ya umma haizuiliki. Hivyo, ndivyo unavyoweza kueleza uamuzi wa mashabiki wa klabu ya Barcelona kukataa jezi mpya za klabu hiyo.


Klabu hiyo ilitangaza jezi mpya Jumanne na kueleza kuwa zitaanza kutumika msimu wa 2015. Hata hivyo, siku mbili baadaye asilimia 78 ya mashabiki wa Barcelona wamepinga jezi hiyo mpya wakidai kuwa inakiuka utamaduni wa miaka 115 wa klabu hiyo.

Wameeleza mashabiki hao katika kura hiyo kuwa uamuzi wa kubadili jezi zenye michirizi na badala yake kutumia hizo mpya haukubaliki.

Wamedai kuwa historia ya miaka 115 haiwezi kufutwa kirahisi na kutokana na hilo, kura zilizopigwa kupitia gazeti la Sport Jumanne zimeonyesha kuwa wengi hawaafiki.

Nalo gazeti la Mundo Deportivo jana liliwanukuu mashabiki wa Barcelona wakieleza kutofurahishwa kwao na mabadiliko hayo.

No comments: