Sunday 30 November 2014

YULE HOUSE GIRL WA UGANDA AANZA KUFUNGUKA....SOMA ALICHOKIONGEA..



Baada ya story za yule msichana anayefanya kazi za ndani Uganda kuchukua nafasi ya pekee katika vyombo mbalimbali vya Kimataifa Duniani, hatimae mdada huyo ameanza kufunguka kwa mara ya kwanza tangu afanye kosa hilo.

Msichana huyo Jolly Tumuhiirwe ambaye kwa sasa amekamatwa na Polisi amesema sababu iliyomfanya amtese mtoto Arnella Kamanzi, ni kutokana na kuchanganyikiwa baada ya waajiri wake kutompatia pesa ili amtumie baba yake ambaye alikuwa anaumwa.

Amesema anajiona mwenye hatia kwa alichokifanya japo anadhani alifanya hivyo kama njia ya kumkanya mtoto huyo kwa kuwa alikuwa akimuona mama wa mtoto huyo akimpiga kama njia ya kumkanya.

Jolly amelalamika kuwa anajisikia vibaya pale ambapo wafungwa wenzake wamekuwa wakimtenga sana na kutaka kumpiga.

No comments: