Thursday, 4 December 2014
188 WAHUKUMIWA KIFO NCHINI MISRI
Mahakama moja ya Misri imewahukumu kifo wafuasi 188 wa harakati ya Ikhwanul Muslimin kwa madai ya kuhusika kwenye shambulio lililotokea mwaka 2013 katika kituo cha polisi mjini Cairo. Hukumu hiyo ilitangazwa hapo jana ambapo watu hao wanadaiwa kushambulia na kuua askari kadhaa wa usalama. Wakati huo huo maelfu ya wananchi wa Misri wameandamana nchini humo kupinga uamuzi wa mahakama wa kumfutia mashtaka yote yaliyokuwa yanamkabili dikteta wa zamani wa nchi nchi hiyo Hosni Mubarak.
Waandamanaji hao huku wakitoa nara za kupinga serikali na kulaani utawala wa kijeshi wa Misri, wamesema kuwa hawatosalimu amri hadi pale matakwa yao yatakapotekelezwa. Polisi ya Misri imefunga barabara zote zinazoelekea katika Meidani maarufu ya mjini Cairo ambako hukusanyika waandamanaji, baada ya kuanza wimbi jipya la malalamiko ya wananchi ya kupinga kufutiwa mashtaka Hosni Mubarak.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment