Wednesday, 3 December 2014

WABADILISHANA WAKE ZAO BAADA YA KUFUMANIANA

Wanaume wawili katika Halmashauri ya Busokelo Wilaya ya Rungwe wamefumaniana na kulazimika kubadilishana wake zao baada ya kufanya makubaliano ya maandishi  yaliyosimamiwa na Serikali ya Kijiji.



Afisa Mtendaji wa Kijiji ambapo limetokea tukio hilo amesema watu hao Paul Mboma alikutwa na Nuru Sangwela, Ambakisye Mwakasege alikutwa na Lusie Lusepo ambapo kila mmoja alikutwa na mke wa mwenzake na chini ya usimamizi wa Mtendaji huyo wakakubaliana kubadilishana ambapo kila mmoja alimchukua mke wake na wakasaini makubaliano hayo.
Wamesema kuwa maafikiano hayo yamefikiwa ili kuepusha urafiki wao usiharibike.

No comments: