Kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey akiifungia timu yake katika ushindi wa 2-4 dhidi ya Galatasaray.
Arsenal ilifunga mabao yake kupitia kwa Aaron Ramsey na mshambuliaji raia wa Ujerumani Lukas Podolski ambapo kila mmoja alifunga mabao mawili .
Katika mchezo mwingine wa kundi D wawakilishi toka ujerumani Borrusia Dortmund walibanwa mbavu wakilazimishwa sare ya 1-1 katika mchezo dhidi ya Anderlecht ya Ubelgiji.
Matokeo haya yanamaanisha kuwa timu za Arsenal na Borrusia Dortmund zimefanikiwa kufuzu hatua ya 16 bora ambapo Dortmund wamefuzu kama washindi huku Arsenal wakishika nafasi ya pili .
Katika michezo mingine iliyochezwa jana usiku Real Madrid walifanikiwa kushinda mchezo wao wa 19 mfululizo katika mashindano yote wakiwafunga Ludogorets toka Bulgaria 4-0 .
Wafungaji wa Real kwenye mchezo huo walikuwa Cristiano Ronaldo , Gareth Bale , Alvaro Arbeloa na Alvaro Medran .
Ushindi huu umewafanya Real wafuzu hatua ya 16 bora kwa kishindo wakiwa wamekusanya pointi 18 baada ya kushinda michezo yote 6 ya kundi lao .
Liverpool ambayo ilikuwa nyumbani ikicheza na Fc Basle iliambulia sare ya 1-1 matokeo ambayo yalikuwa na faida kwa wapinzani wao ambao wanaungana na Real Madrid kufuzu hatua ya kwanza ya mtoano.
Fc Basle imewatoa Liverpool kwenye michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kuwalazimisha sare ya 1-1.
Katika michezo mingine Juventus na Atletico Madrid walitoka sare ya bila kufungana , Olympiakos wakawafunga Malmo 4-2 , Benfica na Bayer Leverkusen nazo zikatoka sare ya 0-0 , huku As Monaco ikishinda dhidi ya Zenith St Petersburg kwa matokeo ya 2-0 .
Kwa matokeo haya timu za Juventus , Atletico Madrid , Monaco na Bayer Leverkusen zinaungana na Arsenal , Dortmund , Real Madrid na Fc Basel kufuzu hatua ya 16 bora .
sare ya 1-1 dhidi ya Atletico Madrid ilitosha kuwavusha Juventus kwenye hatua ya 16 bora.
No comments:
Post a Comment