Thursday, 4 December 2014

KOREA KASKAZINI YAAMURU RAIA WENYE JINA KAMA LA RAIS KUBADILI MAJINA YAO MARA MOJA..


   
Rais Kim Jong Un



Kupitia kituo cha luninga cha taifa hilo KBS,Korea Kaskazini imetoa amri Kali kwa watu wote wanaofanana jina ama majina na rais wa nchi hiyo Kim Jong Un kubadilisha majina yao mara moja...

Sambamba na hilo Korea Kaskazini pia imepiga marufuku matumizi ya majina ya viongozi wake wawili ambao ni baba ake Kim ( Kim Jong II ) na jina la babu yake Kim ( Kim II Sung).....

Jina la Kim Jong Un haliruhusiwi kupewa kwa mtoto yeyote atakaezaliwa nchini humo na wale woooooote wenye jina hilo kwa hivi sasa wanatakiwa waache kulitumia jina hilo na pia wanapaswa wafanye utaratibu wa kubadilisha majina yao kwenye vyeti vyao vya kuzaliwa na kwenye nyaraka mbalimbali kama vile kwenye vitabu vya makazi na vitambulisho mbalimbali...
Imeelezwa kuwa majina hayo ya Kim na Jong ni majina maarufu sana nchini Korea Kaskazini hivyo katazo hilo linasemekana litaumiza raia wengi wa nchi hiyo.....




No comments: