Thursday, 4 December 2014

‘Mrwanda chaguo langu’

Dar es Salaam. Kocha mkuu wa Simba, Patrick Phiri amemrudisha kundini mshambuliaji Danny Mrwanda akieleza kuwa ndiye alikuwa chaguo lake.

Tayari, Mrwanda amepewa na uongozi wa klabu hiyo mkataba wa miezi sita huku kocha huyo Mzambia akiwa hana mpango na kiungo mshambuliaji raia wa Gambia, Omary Mboom.

Phiri alieleza jana kuwa roho yake imesuuzika baada ya Mrwanda kupewa mkataba wa miezi sita wa kuichezea Simba.

Jumatatu iliyopita, Mrwanda alisaini kuichezea timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi huku Phiri akisikitika kumkosa mshambuliaji mwingine wa zamani wa klabu hiyo, Mussa Hassan ‘Mgosi’ aliyeko Mtibwa Sugar.

Phiri aliliambia gazeti hili jana kuwa anamfahamu Mrwanda kwa muda mrefu, yeye ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa, amefurahi kumpata, atamsaidia kwenye safu ya ushambuliaji.

“Natarajia kuwa na safu nzuri ya ushambuliaji baada ya kumpata Mrwanda pia Danny

No comments: