Thursday, 4 December 2014

KOREA KASKAZINI YAISHUTUMU MAREKANI KWA KUTENGENENZA NA KUSAMBAZA VIRUSI VYA EBOLA BARANI AFRIKA


Koreas Kaskazini imeishutumu Marekani kwa kusambaza makusudi virusi vya ugonjwa wa Ebola na kwamba inatengeneza silaha hiyo ya kibailojia ili kuwa taifa lenye nguvu zaidi duniani.


Taifa hilo limelazimika kufunga mipaka yake kuzuia watalii ikiwa ni pamoja na kumtenga kila anayeingia. Ripoti ya Korean Central News Agency (KCNA) inadai kuwa aliyekuwa msaidizi wa Rais wa zamani wa Marekani, Reagan amewataarifu kuwa Marekani ilivumbua seli ya kirusi cha Ebola kwa malengo ya kuanzisha silaha ya kibailojia.

Msaidizi huyo alitajwa kwa jina la Roberts, ambaye gazeti la The Washington Post limesema anaweza kuwa Paul Craig Roberts.

Hivi karibuni Roberts aliandika makala kwenye blog isemayo: ‘Is The US Government The Master Criminal Of Our Time?’ Makala hiyo ilisema kuwa Marekani ilitoa dola milioni 140 kwenye kampuni moja ya dawa kufanya utafiti wa kirusi hicho na kuchagua bara la Afrika kama sehemu ya majaribio.

Makala hiyo ilisema taarifa hiyo ilitolewa na profesa wa Liberia ambaye hakutajwa jina.

Iliongeza kuwa Marekani ilitengeneza kinga ya kirusi hicho lakini ilizuia kujulikana duniani kwa faida yake yenyewe.

No comments: