Saturday 20 December 2014

ELTON JOHN KUOLEWA KESHO


      
Mwanamuziki nguli wa nchini Uingereza, Elton John anatarajia kuolewa katika ndoa ya jinsia moja na mpenzi wake wa siku nyingi aliyedumu naye kwa miaka 20, David Furnish.
       

CHRISTIAN BELLA AVUNJA MAZOEZI YA SIMBA SC

 

MECHI ZA LIGI KUU ENGLAND LEO NA KESHO HIZI HAPA


AMISI TAMBWE AMWAGA MACHOZI HADHARANI BAADA YA KUONA NYUMBA ANAYOISHI MBUYU TWITE...

SIKU chache baada ya aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Mrundi, Amissi Tambwe, ajiunge na Yanga, amejikuta akitokwa na machozi baada ya kutembelea nyumbani kwa beki wa timu hiyo ambaye ni raia wa Rwanda na mwenye asili ya DR Congo, Mbuyu Twite.
Tambwe alikumbwa na hali hiyo bila ya kutegemea kutokana na kujionea maisha mazuri ambayo anaishi beki huyo huku akiambiwa kuwa na wachezaji wengine wa timu hiyo nao wanaishi vizuri kama ‘professional’. 

PLUIJM ASAINI MWAKA MMOJA NA NUSU KUINOA YANGA


       Kocha Mholanzi wa Yanga, Hans van Der Pluijm.
WAKATI kocha Mholanzi wa Yanga, Hans van Der Pluijm akisaini mkataba wa mwaka mmoja na nusu kuinoa Yanga jana, Mbrazili aliyefungashiwa virago, Marcio Maximo juzi usiku alikabidhiwa kitita chake cha dola 12,000 (zaidi ya Sh milioni 20) na kumalizana kabisa na Yanga.
Pluijm aliyetua kuifundisha timu hiyo Jumatatu ya wiki iliyopita, amesaini mkataba huo baada ya Yanga kumalizana na Maximo ambaye wamempa mshahara wake wa mwezi mmoja kama walivyokubaliana kimkataba. 

BAADA YA DIAMOND KUDAI MIMBA ALIZOMPA PENNY ZILIHABIKA KIUTATA! ZILIPENDWA HUYO AFUNGUKA KIIVI!


    
 

FLORA MBASHA AWASILISHA MAHAKAMANI DAI LA TALAKA OMBI LA MGAO WA MALI NA MTOTO

Mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili nchini Tanzania,Flora Mbasha, amekwenda katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar-es-Salaam, akiomba kuvunjwa kwa ndoa yake na mumewe Emanuel Mbasha.
Flora amefungua kesi ya madai namba 64 ya mwaka huu kesi ambayo inasikilizwa na hakimu Maxi, Devota Kisoka. 

WOLPER NA KING MAJUTO NDANI YA BONGE MOJA LA MOVIE


      
Tukiwa unaelekea ukingoni mwa mwaka 2014 , Waigizaji Jackline Masawe “Wolper”na King Majuto wameonekana wakiwa mzigoni kutengeneza kitu kipya. Mwanadada Wolper aliidondosha picha hii na kuandika “New Movie with majuto dady”

MPAMBE WA MGOMBEA URAIS 2015 AFUMANIWA AVISHWA SHANGA...


        
JAMAA anayedaiwa kwamba ni mpambe mkubwa wa mmoja wa wagombea urais mwakani ambaye ni fundi wa kufunga madishi, mkazi wa Magomeni-Makanya jijini Dar es Salaam, almaarufu Mgosingwa, amejikuta akivishwa shanga baada ya kunaswa na mke wa mtu chumbani kwake.
    

Friday 19 December 2014

MAXIMO OOOUUUUTTTT PRUIJM NA MKWASA WARUDI KUINOA YANGA..!!!....

Baada ya kuwepo kwa taarifa zisizothibitishwa rasmi za kufukuzwa kazi kwa kocha mkuu wa timu ya Dar es salaam young African Mbrazil Marcio Maximo, hatimae hii leo uongozi wa timu hiyo umemtangaza rasmi Mdachi Hans Van Der Pruijm kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.

MOVIES ZA KIBONGO KUSHUKA BEI IFIKAPO MWAKANI



Baadhi ya waigizaji na wadau wanaofanya kazi na kampuni ya Steps Entertainment , leo asubuhi walitambulisha bei mpya na muonekano mpya wa DVD covers za filamu zao kwenye ukumbi wa habari maelelzo.

JOKATE NEXT LEVEL...ASAINI MKATABA WA BILIONI 8.5 NA KAMPUNI YA KICHINA KUMTENGENENZEA BIDHAA ZAKE ZA KIDOTI...


                                        

Mrembo Jokate Mwegelo amesaini makubaliano yenye thamani ya Sh8.5 billion na kampuni ya Kichina,  Rainbow Shell Craft Company Limited kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za lebo yake ya Kidoti.

PICHA,KUTOKA CHUMBANI MPAKA UKUMBINI ‘ALLWHITE CIROCPARTY’ ILIYOFANYIKA KAMPALA UGANDA....




 Pati ya Zari ‘AllWhite CirocParty’ iliyofanyika usiku wa kuamkia Decemba 19 mjini Kampala imeisha saa 11 alfajiri, Kwa mjibu Wa wahusika wa club @guvnoruganda wanasema ukumbi wao haujawahi kujaza watu kama ilivyokuwa kwenye party hii, licha ya watu kujaa ndani bado palikuwa na watu walioshindwa kuingia na kubaki nje . 


Zifuatazo ni picha zilizopigwa kuanzia chumbani,Diamond na Zari walipokuwa wakijiandaa hadi ukumbini party hiyo ilipofanyika....
     

JA RULE KURUDI KWENYE GAME MWAKANI

 
Rapper Ja Rule ambaye amekuwa kimya kwenye muziki baada ya kutoka jela amezungumzia uwepo wa album mpya mwaka 2015. Kwenye interview aliyofanyiwa hivi karibuni Ja Rule amesema “ Nina album kama tatu ambazo ziko tayari na nitaanza kutoa single 2015, sitatoa album nzima mapema “ 

Hivi karibuni Ja Rule aliimbwa kwenye wimbo wa Asap Ferg aliofanya na Big Sean uliopewa jina “Ja Rule ” , alipoulizwa kuhusu single hii alisema ” Ni mapenzi ya ukweli huyu jamaa kaonyesha, nilifurahishwa sana na kazi yao wote wawili “


DIAMOND APEWA ULINZI KUTOKA JESHI LA UGANDA- UPDF



 Mlinzi kutoka jeshi la Uganda 

        

VIDEO YA MWANA KUTOKA LEO KUONEKANA KWENYE VITUO VIFUATAVYO

Video iliyosubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki wa Ali Kiba ‘Mwana’itaanza kuonyeshwa ijumaa ya 19 Decemba 2014. Ali Kiba amethibitisha kuwa video imekamilika kwa kutoa kionjo cha video hio na kusema ‘Videoimetayarishwa na muongozaji kutoka Afrika Kusini na imefanyika maeneo ya mjii wa Cape Town” .  

UTATA KIFO CHA AISHA MADINDA HUU HAPA


MENGINE yameibuka! Kifo cha aliyekuwa mnenguaji wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Mwanaisha Mohamed Mbegu ‘Aisha Madinda’ kimeibua mengine ambapo baadhi ya watu wa karibu wanaamini kimetokana na kudungwa sindano tano za majimaji yenye madawa ya kulevya, ‘unga’ na rafiki yake, Ijumaa ‘Kubwa’ linakupa zaidi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, Aisha alidungwa kwa makusudi sindano hizo na rafiki yake mmoja ambaye polisi bado wanamtafuta, ikidaiwa lengo lilikuwa kummaliza.

MJUE AISHA MADINDA KUANZIA KIGOMA,UHOLANZI,DUBAI,DAR HADI UMAUTI....

 
Aisha Madinda Enziza uhai wake.

Amekwenda mapema mno! Siku ya Desemba 17, mwaka huu haikuwa poa hata kidogo kwenye tasnia ya muziki wa dansi Bongo katika kipengele cha unenguaji.Chumba chetu cha habari  kinachofanya kazi kwa karibu na mastaa Bongo kilipata mshtuko wa aina yake.
Zilikuwa ni habari mbaya za kifo cha aliyekuwa mnenguaji bei mbaya wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ inayosimamiwa na Kampuni ya ASET chini ya mkurugenzi wake, Asha Baraka, Mwanaisha Mohamed Mbegu. Wengi tulimzoea kwa jina la stejini la Aisha Madinda. 

NDOA NDOANO: MCHEKI MAIMARTHA ALIVYOZEEKA


Mtangazaji Maimartha Jesse ‘Mai’.
Mtangazaji Maimartha Jesse ‘Mai’ ameibuka na kusema kuwa kitendo cha yeye kuingia kwenye maisha ya ndoa kimemsababisha sasa aonekane kama aliyezeeka kwani mambo mengi ya kisichana ameyaacha. 

THEY CHEAT AGAIN....DIAMOND ANYAKUA TUZO NYINGINE

 

VAN VICKER AWASHANGAA WABONGO

                                             
Mwigizaji na mwongozaji wa filamu wa nchini Ghana, Van Vicker ameshangazwa na vyombo vya habari za udaku za hapa Bongo, kwa kile ambacho kimelipotiwa kuhusu yeye na muigizaji Wema Sepetu.
Kwenye blogs na magazeti mbalimbali ya udaku hapa Bongo zilijaa habari za kuwa Wema na Van Vicker mbali kucheza movie kuna mambo mambo walifanya eti kwa sababu tu Wema ameachana na aliekuwa mpenzi wake Diamond Platnumz na hivyo alitaka kumrusha roho, kitu ambacho hakina ukweli wowote. 

Thursday 18 December 2014

WAZIRI ANNA TIBAIJUKA ASEMA AKIJIUZURU RAIS ATAMSHANGAA...

 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka amegoma kujiuzulu kwakuwa haoni sababu ya kufanya hivyo...  

KANISA LACHAGUA ASKOFU MWANAMKE KWA MARA YA KWANZA


               
Kanisa la Uingereza limemchagua askofu wa kwanza mwanamke.Mchungaji Libby Lane atakuwa askofu wa Stockport mnamo mwezi January ,na kumaliza ukiritimba wa wanaume kuwa maaskofu katika kanisa hilo.Amesema kuwa amefurahishwa na hatua hiyo.Kanisa la Uingereza liliwachagua wanawake mara ya kwanza kama makuhani mnamo mwaka 1994.Wanawake tayari wameruhusiwa kuwa maaskofu katika maeneo mengine ya jamii ya kianglikana ,ikiwemo Marekani na kusini mwa Afrika.

CHANZO: BBC SSWAHILI

Mh.RAIS AKIRI IDADI KUBWA YA WANACHUO UDOM KUWA NI MAKAHABA...

 

DIAMOND AANIKA SABABU ZA KUWAACHA PENNY,JOKATE NA WEMA..


Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' akiwa katika pozi.
KWA mara ya kwanza supastaa ndani na nje ya Bongo kutoka muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewafungukia waliowahi kuwa wapenzi wake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, Wema Sepetu ‘Madam’ na Penniel Mungilwa ‘Penny’ kuwa waligoma kumzalia mtoto.  

WEMA SEPETU AMCHANA KWEUPEEEE ZAMARADI MKETEMA WA CLOUDS ..


Mara baada ya mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi cha maswala ya filamu nchini cha TAKE ONE, Zamaradi Mtetema kuweka bandiko mtandaoni, akiwatata mashabiki na wapenzi wake, wataje mambo matano ambayo niyaukweli kuhusu yeye Zamaradi kwa jinsi wanavyomuona na atatoa zawadi kwa yule atakae patia.  Madam Wema Sepetu alikuwa ni mmoja kati ya watu waliojitokeza kwa kumwambia ukweli bila kumficha wala kusita na kutoa 5 facts za ukweli kabisa... 

HAYA NDIO MAJANGA YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA


HAYA MAJANGA! Wakati vuguvugu la uchaguzi wa serikali za mitaa likiwa bichi, baadhi ya sehemu zikiwa zinasubiri zoezi hilo kutokana na sababu tofauti, matukio mbalimbali, yakiwemo ya kusikitisha, yameripotiwa. 
 Wananchi wakiutoa mwili wa marehemu Bandoma Mabele (58) majini.

Huku washindi wa nafasi mbalimbali zilizokuwa zikigombewa wakisheherekea kwa namna ya aina yake, katika Kijiji cha Mwagika, Sengerema mkoani Mwanza, kulitokea msiba wa kusikitisha, baada ya mgombea wa nafasi ya Uenyekiti, aliyetambulika kwa jina la Bandoma Mabele (58) kufariki dunia kufuatia kuzama ndani ya maji ya ziwa Victoria. 

BI.CHEKA ANAHITAJI MSAADA WA HARAKA


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Bi Cheka hivi sasa ni mgonjwa. Anahitaji matibabu na huduma muhimu kutokana na umri wake mkubwa 
(ana miaka 55).
Hali yake kimaisha ni mbaya, kwani anaishi katika kibanda cha udongo, yeye na wajukuu zake. Global Publishers inaendesha harambee hii ili aweze angalau kujenga kibanda cha bati na kupata matibabu. 

Mchangie chochote ulichonacho, iwe 500, 1000, 5000 au zaidi kupitia namba 0654 880 707. Kitakachopatikana mtatangaziwa. Kutoa ni Moyo!

Wednesday 17 December 2014

TETESI:BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA...


Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri. Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa leo jioni yamewatupilia mbali watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji. 

Waliotupwa nje kutokana na tuhumua za ufisadi ni pamoja na Anna Tibaijuka- aliyekuwa waziri wa ardhi nyumba na makazi, Sospeter Muhongo-aliyekuwa waziri wa nishati na madini huku Lazaro Nyalandu akihamishwa kutoka wizara ya mali asili na italii aliyokuwa akihudumu. 

Walioondolewa kwenye wizara zao za awali na kuhamishwa ni pamoja na Lazaro Nyalandu ambaye anarudi mazingira. Saada Mkuya Salum kutoka fedha na kuhamishiwa ikulu pamoja na Gaudensia Kabaka.Hayo ni baadhi ya majina niliyopata. 

UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA: AFUKUZWA BAADA YA KUMSHINDA BABA MWENYE NYUMBA


VITUKO vinazidi kuripotiwa katika chaguzi za serikali za mitaa zinazoendelea nchini na mjini Morogoro, mgombea kutoka muungano wa Ukawa, Sharrif Abdul Mnola (Chadema) ametimuliwa kwenye nyumba aliyokuwa anaishi baada ya kumshinda mpinzani wake, Makalla Salum Hassan (CCM) ambaye ni mmiliki wa mjengo huo uliopo mtaa wa Ngoma ‘A’ kata ya Mji Mpya.
Sharrif ambaye ni dalali wa magari alishinda baada ya kupata kura 79 huku Makalla akipata 72. 

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AJIUZURU..SOMA SABABU ALIYOTOA..


         
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amejiuzulu nafasi yake hiyo kuanzia jana,Jumanne, Desemba 16, 2014 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amekubali ombi hilo la kujiuzulu.

Katika barua yake kwa Mhe. Rais Kikwete, Jaji Werema amesema kuwa ameomba kujiuzulu kwa sababu ushauri wake kuhusiana na suala ya Akaunti ya Tegeta Escrow hakueleweka na umechafua hali ya hewa.
Mhe. Rais Kikwete amemshukuru Jaji Werema kwa utumishi wake ulioongozwa na uaminifu na uadilifu.

Tuesday 16 December 2014

MAISHA HAYANA KANUNI...JOHARI AAMUA KUWA MUUZA NDIZI..MWENYEWE AFUNGUKA..


     
Muigizaji mkongwe wa filamu, Blandina Chagula ‘Johari’ amabae pia ni mkurugezi wa kampuni ya RJ ambayo inajihusisha na utengenezaji wa filamu hapa nchini.

MTUHUMIWA WA WIZI WA PIKIPIKI ANUSURIKA KUUAWA MAGOMENI LEO HII....


                                   


 KIJANA ambaye jina lake haikufahamika mara moja, amenusurika kuuawa na wananchi wenye hasira kwa tuhuma za wizi wa pikipiki jijini Dar.Tukio hilo la kusisimua limetokea asubuhi ya leo Magomeni-Mwembechai, ambapo lilisababisha foleni ndefu ya magari wakati kijana huyo akiadhibiwa na wananchi.

MISS TANZANIA HATARINI KUSITISHWA....

Hatma iwapo mashindano ya Miss Tanzania yataendelea au yatasitishwa kwa muda, itategemea majibu ya tathmini iliyofanyika mwishoni mwa wiki jana yanayotarajiwa kutolewa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) wiki chache zijazo.  

DIAMOND ASINDIKIZWA NA MAGARI YA POLISI KWENDA AIRPORT HUKO MOMBASA

Diamond akisindikizwa Airport  Kwa Msafara wa Polisi Huko Mombasa 

YULE HOUSEGIRL WA UGANDA ALIEMTESA MTOTO AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 4

Jolly Tumuhirwe apatikana na hatia ya kumtesa mtoto mdogo na kufungwa jela miaka 4
Yaya wa Uganda aliyejipata pabaya kwa kumchapa mtoto wa mwajiri wake, amehukumiwa jela miaka minne kwa kosa la kumtesa mtoto. 

DIAMOND AKANUSHA KUWANYANYASA WASANII WENZAKE HUKO MOMBASA

Nimesikitishwa Sana na habari zilizoandikwa na moja ya chombo cha habari, kuwa eti nliwanyanyasa wasanii wenzangu Nyota ndogo na Susumila, kwa kuwafukuza kwenye VIP lounge na sijui eti niliwazuia wasitumie maji ya chupa hivi inaingia akilini kweli hii!!!??  
 

Monday 15 December 2014

WEMA SEPETU ALICHUKIA NA KULITELEKEZA GARI ALILOZAWADIWA NA DIAMOND....



Ndinga aina ya Nissan Murano alilozawadiwa supastaa Wema Sepetu na aliyekuwa mchumba wake, Nasibu Abdul ‘Diamond'.

HII NDIO KAULI YA KWANZA YA HAPPINESS WATIMANYWA BAADA YA KUTOFANIKIWA KUTWAA TAJI LA MISS WORLD

Baada ya Miss South Africa anajulikana kwa jina la  Rolene Strauss ambaye ndie mshindi wa taji la  Miss World 2014, Aliyekuwa akiwakilisha Tanzania kwenye michuano hiyo kupitia mtandao ya kijamii wa Instagram amefunguka baada ya kushindwa kunyakua taji hilo na hichi ndicho alichokiandika

MATOKEO KAMILI MISS WORLD HAYA HAPA

Yafuatayo ni matokeo kamili ya miss World yakijumuisha ile TOP 25 pamoja na matokeo ya events challenges...
       GRAND MISS WORLD RESULTS

MISS TANZANIA AWA WA PILI ON MISS WORLD PEOPLE'S CHOICE AWARD



                               
 

Hakika lile zoezi la uhamasishaji wa kumpigia kura mrembo wa kutoka Tanzania Happiness Watimanywa limezaa matunda mara baada ya kumuwezesha mrembo huyo kushika nafasi ya pili katika kipengele hicho cha kupigiwa kura......

Licha ya kushika nafasi hiyo,muwakilishi wetu huyo hakuweza kupata nafasi ya kuingia kwenye kumi bora ya mashindano hayo makubwa ya urembo duniani kwani mshindi wa kwanza ndie hupata nafasi ya kuingia 10 bora ama 11 bora kama ilivyokuwa kwa mwaka huu ambapo miss Thailand alipata nafasi hiyo baada ya kuibuka namba moja kwenye kipengele cha Miss World People's Choice...
           

LICHA YA SKENDO ZAKE...HUU NDIO UTAJIRI WA ZARI THE BOSS LADY


Maneno ya zari akifunguka na kuwaelezea mashabiki wake jinsi ya utendaji kazi wake, wa nguvu na namna ulivyompa mafanikio, na hii ndio kauli ya zarithebosslady in other business news….

When you hustle hard daily, & stay focused on your vision motivation will never be an issue.

Check out my jewellery store at garden city shopping mall for wedding, engagement rings and all your other fashion jewellery…. 

Sunday 14 December 2014

HABARI KUTOKA MISS WORLD: KUMBE WATANZANIA TUKIAMUA TUNAWEZA MPAKA SASA WATIMANYWA YUKO NAFASI YA PILI


Watanzania wameamua kwamba tukiamua tunaweza, good news kutoka London Uingereza, ambako yanafanyika mashindano ya Miss World mwaka 2014.Happiness Watimanywa, mwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano hayo ameshare na sisi taarifa nyingine nzuri kupitia ukurasa wake wa Instagram.Happiness kaandika hivi; “Hey guys. Siwezi amini kuwa tumefika namba 2. Tuongeze bidii maana nchi nyingine pia wako bize na kura. Lets do this Tanzania!!!! Naamini pamoja tutafika. #votevotevote #PigaKuraSasa#DownloadTheApp#HuuNiMwakaWetu“– @happinesswatimanywa

MSANII BONGO MUVI ATAKA KUJIUA KISA YANGA KUCHAPWA NA SIMBA.....

Baada ya Simba kumshushia kipigo kikali Yanga  cha mabao mawili kwa sifuri, nakuibuka mtani jembe. Muigizaji na shabiki mkubwa wa timu ya Yanga, Mchopanga  inasemekana alitaka kumeza madawa baada ya kuchapa kilaji.