Saturday, 24 January 2015

WEMA SEPETU AKANUSHA KUMDAI DIAMOND MILIONI 10...

 
Kumekuwa na stori kibao tangu Wema sepetu kuachana na Diamond platnumz,lakini kilicho make head lines zaidi ni hii ya Wema Sepetu kumfungulia Diamond mashtaka ya kumdai.
Kwenye interview aliyo ifanya baada ya kuzagaa kwa taarifa hizo za kufungua mashtaka kwaajili ya kumstaki mpenzi wake wa zamani,wema hapa anafunguka.... 

TAZAMA MCHUNGAJI AKIMFANYIA MAOMBI MWANAMAMA...NI HATARI...

Wanawake MUNGU awasaidie sana Mjue kujenga Mahusiano binafsi ya karibu na MUNGU mwenyewe kuliko kutegemea sana kuombewa hovyo hovyo,Kisa tu Umeambiwa na Rafiki yako kwamba yuko Apostle flani ana Upako sana. 

SAHAU KUHUSU MASOGANGE,KUTANA NA NKEM KUTOKA NIGERIA,NI BALAAA

BABA NA MAMA DIAMOND WAKO HOI KITANDANI,WAFICHWA WASIONEKANE

                                      
Wazazi wa nyota wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kasim na Abdul Juma wako hoi vitandani wakikabiliwa na maradhi mbalimbali...
TUANZE NA MAMA DIAMOND.. 
                           

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha uhakika, mama Diamond hajiwezi kwa mwezi mmoja sasa akisumbuliwa na maradhi yenye kuashiria kupooza sehemu ya mwili na kushindwa kutembea. Anaugulia nyumbani kwake, Sinza ya Mori jijini Dar es Salaam.
YADAIWA KUWA SIRI
Habari zinadai kuwa, ugonjwa wa mama huyo umefanywa kuwa siri kwa watu wengine lakini bila kujulikana kisa cha usiri huo.

PENZI LA JACKLINE WOLPER NA NEY WA MITEGO,MAMBO HADHARANI,UKIBISHA UNA MATATIZO YAKO BINA

BAADA ya kudaiwa kuwa wapenzi na kisha habari hizo kufifia, hatimaye penzi la mwigizaji wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper na Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, limeibuka upya ambapo safari hii Nay ameamua kufunguka hadharani..

WEMA SEPETU AATHIRIKA KWA KOPE BANDIKA,MWENYEWE AELEZA MAZITO

 
BEAUTIFUL Onyinye, Wema Sepetu ‘Madam’ amefunguka kuwa anajuta kutumia kope za bandia kwa muda mrefu kwani zimemua

MWANAMKE AKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA YA SH BILIONI 2.5 NYUMBANI KWA MBUNGE

MWANAMKE mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Doreen John Mlemba, mwenyeji wa Same mkoani Kilimanjaro, mwishoni mwa mwaka uliopita alikamatwa kwa kuhusishwa na shehena ya madawa ya kulevya aina ya Heroin, yenye thamani ya shilingi bilioni 2.5.

SIRI YA WANAWAKE WENYE MWANYA,NDEVU NA KIDOTI CHEUSI YAJULIKANA...

                                                       
 Ushawahi kumuona mdada au mwanamke mwenye mwanya,ndevu au kialama cheusi maarufu kama kidoti???? 
Ka ma wewe ni kijana na bado hujaoa au unamchumba mwenye vitu hivyo vitatu,basi usimuache,kwanini Usimuache????  

BANZA STONE YU MAHUTUTI MJINI TUNDUMA,WASAMARIA WEMA KUJITOLEA KUMRUDISHA DAR

 
Walikwenda mkoani Mbeya na bendi yao Rungwe Music Band (zamani Wana Extra), bendi ikasambaratikia huko kila mtu akarejea Dar na hamsini zake, Banza akaamua kwenda Tunduma na huko ndiko balaa lilipomkumba.
Pengine bado uko kizani. Ni kwamba mwanamuziki nyota wa dansi Ramadhani Masanja “Banza Stone” yuko mahututi mjini Tunduma na hana huduma yoyote ya kimatibabu. 

Friday, 23 January 2015

MASOGANGE ATUHUMIWA KUTUMIA INSTAGRAM KUJIUZA HUKO SAUZI

     
MIEZI michache tangu ahamishie makazi yake nchini Afrika Kusini, modo aliyetikisa Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ametia aibu kutokana na kudaiwa ‘kujiuza’ kwa njia ya mtandao nchini humo. 

STATUS TATA ZA WOLPER ZAZUA GUMZO MITANDAONI


Mrembo na mwigizaji mwenye mvuto wa aina yake, Jackline Massawe “Wolper” toka jana amekuwa anaachia picha na jumbe mbalimbali mtandaoni zenye maneno mazito ambayo yamepelekea wengi kuhisi labda kuna kitu kimemkuta mwanadada huyu na sasa ameamua kupunguzia” stress” zake mtandaoni, huku wengine wakamini kuwa hizi ni jumbe za kawaida tu na hakuna kinachomsibu.

AGNESS MASOGANGE AMSHUKURU BELLE 9


Finally video queen maarafu wa Tanzania Agness masogange amefunguka kuwa bila ya belle 9 leo asingekuwepo hapo, coz huko alipo southafrica fursa nyingi zimeshaanza kufunguka na kuanza kutumiwa message nyingi huku wasanii wengi
wakitaka kufanya nae kazi na kuwasaidia wasanii hao kuwataftia ma model wengine, itakumbukwa nyimbo ya masogange ni nyimbo ambayo iliimbwa na belle 9 na kumfanya mwanadada huyo ajulikane all over the east africa na baadhi za nchi za africa..

KUTANA NA KIKONGWE WA MIAKA 90 ANAESOMA SHULE YA MSINGI


Akiwa na umri wa miaka 90 mwanamke wa Kenya ambaye anahudhuria masomo akiwa na wajukuu zake wapatao sita inaaminika ndiye mwanafunzi mzee zaidi anayesoma shule ya msingi duniani.
Akiwa ameketi dawati la mbele kabisa darasani ,yuko darasa la tano na amevalia nguo za shule , Priscilla Gogo Sitienei anamsikiliza mwalimu anayefundisha kwa makini hukua akiandika majina ya wanyama kwa kiingereza kwenye daftari lake. 

UTAFITI: MWANAMKE KUWA JUU YA MWANAUME WAKATI WA KUJAMIIANA NI HATARI KWA MWANAUME

Wanasayansi nchini Brazil wamefanya utafiti ili kubaini ni mtindo upi katika ufanyaji tendo la ndoa ulio hatari zaidi kwa mwanaume.
Kwa mujibu wa utafiti huo, mtindo ambao mwanamke anakuwa juu ya mwanaume ndio hatari zaidi na huwa na risk kubwa zaidi ya kusababisha hata kuvunjika kwa uume.

DIAMOND ATINGA KWENYE TOP TEN ZA TRACE TV YA UFARANSA


Post  hii  ni  maalumu  kwajili  yako  mpendwa  msomaji kama ulikuwa na hamu ya kufahamu video za Afrika zinazofanya vizuri duniani na iliyofanikiwa kuchukua nafasi kwenye countdown za nchi kubwa.

WAGOMBEA UDIWANI KUPIMA VIRUSI VYA UKIMWI KABLA YA KUCHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA NAFASI HIYO


MADIWANI wa Halmashauri ya Nsimbo wilayani Mlele katika mkoa wa Katavi wameshauriwa kupima afya zao ili kubaini kama wana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) kabla ya kuchukua fomu za kugombea nafasi ya udiwani katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwaka huu.

JULIANA KANYOMOZI ATOA YA MOYONI KUVUJA PICHA ZA UCHI MITANDAONI...

 Muimbaji wa Uganda, Juliana Kanyomozi amefunguka kwa urefu kuhusiana na masuala mbalimbali kwenye mahojiano aliyofanyiwa na mtandao wa SatisfashionUG.

ZARI KUWA NA MIMBA,INA MAANA DIAMOND ALIFANYA MAPENZI BILA YA KINGA,JE WALIPIMA LINI NA WAMEJUANA KWA MUDA GANI?????


Takribani wiki nzima sasa mitandaoni kumejaa hii habari ya kuwa shemeji na wifi yetu Zari the boss lady yu mjamzito,ambapo muhusika wa ujauzito huo ni Diamond...Nimekuwa nikijiuliza mwenzenu,Ili mtu aweze pata ujauzito kwa njia ya kujamiiana basi ni lazima afanye mapenzi bila kutumia kinga ya aina yoyote ile hususani Condom.. 
Hivyo kama kweli Zari ana mimba hii ina maanisha walifanya mapenzi kavu kavu na hapa ndipo ninapojiuliza mimi mwenzenu ZARI NA DIAMOND WALISHAPIMA AFYA ZAO??? WAMEJUANA KWA MUDA GANI MPAKA WAFIKIE UAMUZI HUO WAKUTEMBEA PEKU PEKU????  

Thursday, 22 January 2015

ZIFAHAMU CLUB KUMI TAJIRI BARANI ULAYA,REAL MADRID YAFUNIKA


Real Madrid imeibuka kama klabu tajiri zaidi ulaya kulingana na orodha iliyotolewa na Deloitte Football Rich kwa miaka kumi mfululizo.
Manchester United imetoka nafasi ya nne hadi ya pili katika orodha hio, kulingana na mapato ya msimu wa 2013 -2014
Bayern Munich, Barcelona na Paris St -Germain walifuatana kwa orodha hiyo kutoka nambari tatu.
Klabu za Uingereza, Machester City, Chelsea, Arsenal na Liverpool wanafuatana kutoka nambari sita hadi tisa, wote wakionyesha dalili nzuri za kuongeza mapato .

MASKINI RACHEL,AFUATA NYAYO ZA RAY C NAE SASA ALISHWA UNGWA NA KUVUTISHWA BANGI


Kama ilivyotokea kwa msanii nyota wa kike wa bongo fleva, Rehema Chalamira 'Ray C' kuingizwa katika matumizi ya dawa ya kulevya na mtu ambaye alitokea kumwamini sana, ndivyo ilivyotokea sasa kwa msanii anayefuata nyendo zake, Winfrida Josephat 'Rachel' ambapo anadaiwa kuvutishwa unga bila kujua.... 

CSKA MOSCOW YAMUONGEZEA MUDA MBWANA SAMATTA,LIST YA TIMU ZINAZOMTAKA HII HAPA...

 Hatimaye nyota ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe Mbwana Samatta imeanza kung’ara katika anga ya kimataifa ya soka.Taarifa zilizothibitishwa ni kwamba mshambuliaji huyo yupo kwenye majaribio katika klabu ya CSKA Moscow – moja ya klabu kubwa kabisa nchini Urusi ambayo kwa miaka kadhaa imekuwa ikitawala soka la nchi hiyo na kucheza katika michuano ya mabingwa wa ulaya. 

JOKATE AMFUNIKA LULU,MWENYEWE AFURAHIA

 Mwanamitindo na dairekta wa lebo ya Kidoti, Jokate Mwegelo 

MWANAMITINDO na dairekta wa lebo ya Kidoti, Jokate Mwegelo amekuwa tishio kwa msanii wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwa urembo na muonekano katika picha zinazoonekana mitandaoni nchini. 

MASIKINI TAMBWE ASIMULIA ANAVYONYANYASIKA,YANGA YAKIMBILIA TFF KUSHTAKI


Klabu ya Yanga imepanga leo kuwasilisha malalamiko yao juu ya tukio la kunyanyaswa kwa mshambuliaji wake Amissi Tambwe kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lakini pia mchezaji husika amefafanua kwa kina juu ya manyanyaso anayoyapata.

KUFUATIA SAKATA LA ESCROW,WAZIRI MUHONGO,NGELEJA MWAMBALASWA WAJIUZURU NAFASI ZAO....


WENYEVITI wa Kamati za Kudumu za Bunge, waliopendekezwa kuwajibishwa na Bunge hilo katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow, wamejiuzulu nyadhifa zao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Spika Anne Makinda aliwaambia waandishi wa habari katika Ofisi ndogo ya Bunge, waliotaka kujua hatima ya wenyeviti hao, kuwa hawapo tena katika nafasi zao baada ya kujiuzulu.

Wednesday, 21 January 2015

DIAMOND NOMA,AWEKA APPLICATIONA YAKE MWENYEWE GOOGLE PLAY....


  

Star wa Muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz bado anazidi kuongeza wigo wa kutoboboa kimuziki hasa kwa soko la ki mataifa,kwani hivi sasa ameweza kuwa amefikia hatua ya kuwa ana miliki application yake mwenyewe ya google play.  

BWANA NA BIBI HARUSI WAFANANA WAVAA WOTE MAGAUNI,PADRI ACHANGANYIKIWA AGOMA KUFUNGISHA NDOA


Bwana harusi ambaye siku ya harusi yake alivaa gauni kama bibi harusi, kufanana kwao kulizua utata, nani mwanaume na nani mwanamke, ilibidi hata vyeti vya kuzaliwa viletwe ili kumaliza utata huo. 

HUYU NDIO MTUKUTU BALLOTELI

                             

Mario Balotelli ni mchezaji wa Liverpool alipost picha hii kwenye page yake ya Instagram akiangalia timu yake kupitia tv akiwa nyumbani.   

AUNTY EZEKIEL AMSHANGAA KING MAJUTO KUKATAA KUSHIRIKISHWA KWENYE FILAMU ZA WASANII WENZAKE

                                          
Msanii wa filamu Bongo, Aunty Ezekiel.
WAKATI mkongwe wa filamu za kuchekesha, King Majuto akidai kutoshiriki kazi na msanii yeyote kutokana na kuibiwa, msanii mwenzake, Aunty Ezekiel amechukizwa na uamuzi huo.Akizungumza na Uwazi, Aunty alisema kuwa haamini kama wezi wa kazi zake ndiyo chanzo cha Majuto kuachana na filamu za kushirikishwa bali inawezekana kuna tatizo lake lingine.

RASI ANYOLEWA BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA JIJINI DAR ES SALAAM


    

MWANAUME mwenye imani ya Kirasta ambaye jina lake halikuweza kunaswa mara moja, mwishoni mwa wiki iliyopita alijikuta akinyolewa rasta zake bila ridhaa yake kufuatia kudakwa akidaiwa kutaka kuiba kwenye duka moja.

UTATA MPYA KUHUSU MIMBA YA ZARI HUU HAPA


      
Wakati staa mkubwa wa muziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akichekelea kitendo cha mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’ au ‘The Boss Lady’ kunasa mimbayake, habari ya mjini huko Kampala, Uganda ni juu ya aliyekuwa mume wa mwanamama huyo, Ivan Ssemwanga kufunguka na kusema: “Naapa Zari hawezi kuzaa na Diamond.”

Monday, 19 January 2015

RONALDO (CR7) AACHANA NA MPENZI WAKE WA SIKU NYINGI

         

SIRI imefichuka!. Cristiano Ronaldo alisherehekea mwaka mpya peke yake baada ya mchumba wake, Mrusi kutokwenda katika sherehe ya siri aliyoandaa nyumbani kwao Madeira, gazeti maarufu la Ureno la Correio da Manha rimeripoti. 
Gazeti hilo limetoa habari jana na kuthibitisha kuwa familia ya Ronaldo imevunjika baada kukosekana kwa maelewano baina ya Ronaldo na mpenzi wake Irina. 

MWIZI WA AKAUNTI ZA AY NA FID Q HUYU HAPA,NI MTOTO WA MBUNGE...

                                             
Ahmed Mundhiri, kumbe ni mtoto wa Mbunge wa zamani wa Mchinga Mh. Mdhihiri Mdhihiri amekamatwa jana kwa kuiba account za watu mbali mbali kwenye mitandao wakiwemo Fid Q na AY kama anavyoonekana aliponaswa jana live!!

SIR NATURE KUGOMBEA UBUNGE TEMEKE

                           

Msanii nguli wa kizazi kipya Juma Kasim kiroboto almaarufu Sir Nature ametangaza rasmi nia ya kugombea ubunge jimbo la temeke.  

Sunday, 18 January 2015

MCHUNGAJI MTIKILA AMSHTAKI ASKOFU MOKIWA BAADA YA KUMSHIKA MAKALIO ADAI FIDIA YA BILIONI MOJA


Mchungaji Christopher Mtikila amefungua kesi katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kumshitaki Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican Tanzania Dk. Valentino Mokiwa.
Msingi wa kesi ni kwamba Askofu Mokiwa alimshika makalio Mtikila na kwamba kitendo hicho kilichotokea Juni 25 mwaka jana walipokutana maeneo ya Ilala, kimemdhalilisha.
Mtikila alikuwa ameitwa na Askofu kujadili tamko la la Mtikila kwamba Kanisa la Anglican linajihusisha na ufisadi, ukiwemo wizi wa vifaa vya Hospitali ya Mission ya Millo iliyoko Ludewa mkoani Njombe. 

DIAMOND NA KIBA WAKUTANA UKUMBINI,WACHUNIANA....

     
Kama ulikuwa unaamini kuwa lile bifu la wakali wawili wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Saleh Kiba, limekwisha, basi utakuwa utakuwa unakosea na kujidanganya vibaya mnooooo.....Bifu bado lipo na hii imegundulika baada ya jamaa hao kukutana ukumbini na kuchuniana. 

LULU: SICHANGANYI MADAWA KAMA WENGINE,NITABAKI KUWA MUIGIZA


MTOTO mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema katika maisha yake ya sanaa hataweza kuchanganya madawa kufanya kazi nyingine mbali na kuigiza kama ambavyo wasanii wengine wanafanya. 

AMINI USIAMINI,MJI WA DUBAI UNAONGOZA KWA UAMINIFU SOMA TAARIFA HII...

Dubai imejinyakulia sifa ya kipekee katika kupima Imani za jamii kwa pochi iliyoangushwa mtaani,na mara ikarejeshwa kwa mhusika mara moja. 

Katika utafiti uliofanywa na mtengeneza Filamu mwenye asili ya Uingereza katika mitaa ya Dubai, alijaribu mara arobaini na tano kuidondosha kwa makusudi na katika kila tukio msamaria aliyeiokota aliirejesha pochi hiyo kwa mmiliki wake. 

SALUNI INAYOTOA HUDUMA YA NGONO YAGUNDULIKA KINONDONI,WADADA WA KISOMALI NDIO WAHUDUMU,BEI NI TSHS 60,000 KWA TENDO..

 
Wakati suala la ajira likiwa bado ni kitendawili kikubwa kwa serikali, Jiji la Dar hivi sasa linatisha, baada ya watu kubuni mtindo mpya wa kujipatia fedha kwa kujihusisha na biashara haramu ya ngono katika maeneo yanayotambulika kufanya shughuli nyingine halali.