Wednesday, 3 December 2014
VINARA MAUAJI YA WANAWAKE DAR,WAKAMATWA
Zaidi ya Wanawake 11 wameuawa Dar es Salaam katika kipindi cha miaka miwili na kutupwa barabarani au mitaroni huku miili yao ikiwa imefanyiwa vitendo vya unyama na udhalilishaji.
Kutokana na mauaji kuendelea, Polisi wamefanikiwa kuwakamata watu wawili akiwemo ABOUBAKAR KASSANGA Mkazi wa Mwenge na EZEKIEL ASENEGALA mkazi wa Tandika Dar es Salaam ambao wamekiri kuhusika na vitendo hivyo ndani ya kipindi cha miaka miwili.
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SULEIMAN KOVA amesema baada ya kuwahoji watuhumiwa hao ambao pia wamekiri kuwauwa wasichana wawili hivi karibuni waliotajwa kwa majina ya WANZE MAKONGORO na JACKLIN MASSANJA wamesema wamekuwa wakiwalaghai wasichana kimapenzi na badae kuwaua.
Katika hatua nyingine Kamishna KOVA ametoa tahadhari kwa wasichana kuacha tabia ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi wa ghafla na watu wasiowafahamu ambapo tukio la mauaji ya wasichana hao wawili lilitokea Novemba 19 mwaka huu ambapo baadhi ya vitu vinavyosadikiwa kuwa vya wasichana hao vimekutwa mahala wanapoishi watuhumiwa hao.
Kamishna KOVA amesema upelelezi bado unaendelea ili kuunasa mtandao mzima wa uhalifu huo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment