Saturday, 6 December 2014
HAYATI MZEE MANDELA ATIMIZA MWAKA MMOJA
Wananchi wa Afrika Kusini wamekusanyika katika maeneo mbalimbali ya nchi kukumbuka mwaka wa kwanza tangu kufariki dunia shujaa wa mapambano ya ubaguzi wa rangi, hayati Nelson Mandela.
Mjini Pretoria, mke wa mwendazake Mandela, Bi. Winnie Mandela, amesema ingawa baba wa taifa hilo ametangulia mbele ya haki, athari zake bado zinaendelea kuonekana na zitaendelea kuwanufaisha watu wa kizazi cha sasa na hata wale wa vizazi vijavyo.
Maombi, majonzi na vilio vimetanda katika mji wa Qunnu alikokuwa akiishi Madiba lakini pia watu wa Soweto ambako pia kunahesabiwa kuwa nyumbani kwa Mandela wanaomboleza na kuhuzunika katika siku hii ya kukumbuka mwaka mmoja tangu kifo chake.
Nelson Mandela ambaye alikuwa rais wa kwanza Mwafrika tangu kuanguka utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini alifariki Disemba 5 mwaka uliopita akiwa na umri wa miaka 95.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment