Friday 28 November 2014

NCHI NYINGI ZA AFRICA KUTOFIKIA MALENGO YA MILLENIA


Nchi nyingi za bara la Afrika hazitaweza kufikia malengo ya milinia ifikapo mwaka 2015 kutokana na mwanya uliopo kati ya uchumi na maendeleo ya kibinadamu. Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya kila mwaka ya Umoja wa Mataifa juu ya nchi zenye maendeleo madogo, iliyowasilishwa Alhamisi.

Licha ya kukua kwa uchumi barani Afrika nchi nyingi hazitafikia malengo ya milinia (MDGS) mwakani. Afisa wa maswala ya kiuchumi kwa Afrika katika Umoja wa Mataifa Junior Davis anasema nchi nyingi za Afrika  hazijaweza  kutumia maendeleo ya kiuchumi kufanya mabadiliko  katika sekta zake za miundo mbinu.


Ripoti hiyo inataja nchi za Ethiopia, Rwanda, Uganda na Malawi kama nchi nne pekee za Afrika ambazo huenda zikafikia malengo hayo ya milenia  kwa sababu zimewekeza katika sekta za maendeleo, miundo mbinu, afya na elimu.

 Nchi ambazo ziko nyuma sana kimaendeleo ni Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambako maswala ya kiutawala bado ni tatizo na zitategemea uungaji mkono wa jamii ya kimataifa kufikia maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Miongoni mwa nchi 48 zisizo na maendeleo makubwa duniani, 34 zimo barani Afrika lakini tatu zimeondoka kwenye orodha hiyo, nazo ni Botswana, Cape Verde na Samoa.

No comments: