Thursday 27 November 2014

MAITI ZA WALIOKUFA KWA EBOLA ZATUPWA HOVYO MTAANI


Wahudumu wa Afya nchini Sierra Leone waliopewa kazi ya kuzika maiti za wagonjwa waliokufa kwa ebola wameamua kuitupa miili hiyo mitaani kutokana na kulalamikia posho ndogo wanazolipwa na Serikali ya nchi hiyo.
Katika kitendo cha kushangaza waliamua kutupa miili 15 ya maiti hizo katika mitaa mbalimbali kwa lengo la kuelezea hisia zao za kuchoshwa na malipo madogo wakati wanafanya kazi kubwa.
Wafanyakazi hao waliripotiwa kukaa siku saba bila kulipwa fedha zao ambapo kwa wiki hulipwa dola100 ambazo walidai ni ndogo ukilinganisha na kazi waliyokua wakifanya kudai inahatarisha maisha yao kwa kiasi kikubwa.
Nyongeza ya fedha hizo walizokua wakitaka ni kwa ajili ya kufidia kazi wanazofanya kwa sababu hufanya katika mazingira magumu ya kuzika wagonjwa wa Ebola ambao huambikizwa kwa njia ya kugusana.
Kituo cha kitaifa kinachosimamia ugonjwa wa Ebola nchini humo kilitangaza rasmi kuwa wafanyakazi wote walioshiriki katika mgomo huo watafukuzwa kazi.

No comments: