Thursday, 20 November 2014
SHY ROSE BHANJI AMTANDIKA MANGUMI MBUNGE MWENZAKE
Mbunge wa bunge la Afrika Mashariki Shy-Rose Bhanji ameingia katika mgogoro mpya baada ya kutuhumiwa kumpiga mbunge mwenzake kutoka Tanzania Kessy Nderakindo jijini Nairobi,Kenya.
Bhanji ambaye amekua katika mgogoro na wabunge wenzake kwa kipindi cha miezi miwili sasa anadaiwa kumvamia Dk,Kessy na kumpiga mgongoni wakati kikao cha bunge hilo kilipoahirishwa.
“Kwa kuwa muda wa bunge ulikua umeisha nisingeweza kuipeleka kesi hiyo bungeni,badala yake kwa kuwa ni shambulizi nikaambiwa niende kuripoti kituo cha polisi cha Bunge ambapo baadaye nilipatiwa cheti cha matibabu”alisema Dk Kessy.
Hadi tukio hilo linatokea hakua amewahi kukwaruzana na Mbunge huyo zaidi ya kushangaa akimvamia na kusema baada ya kumvamia hakupata madhara ya hapo hapo kama alama ama damu ila anasikia maumivu katika sehemu alizompiga.
Bhanji hakupatikana kwenye simu yake na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment