Friday, 21 November 2014
11 WAPOTEZA MAISHA KANISANI
Polisi ya Zimbabwe imetangaza kuwa kwa watu 11 wamepoteza maisha kutokana na msongamano mkubwa wa watu, wakati walipokuwa wakitoka katika uwanja mmoja baada ya kumaliza ibada ya Kikristo. Shadreck Mubaiwa, Msemaji wa Polisi ya nchi hiyo amesema kuwa, watu wanne walifariki katika eneo la tukio huku wengine saba wakipoteza maisha hospitali. Ameongeza kuwa, mauaji hayo yalitokea jana usiku katika mji wenye kuchimbwa madini wa Kwekwe, yapata kilometa 220 kutoka Harare, mji mkuu wa Zimbabwe wakati idadi kubwa ya watu walipokuwa wakitoka katika uwanja wa mji huo kwa ajili ya ibada. Watu wengine wamejeruhiwa na wengine hali zao zikiwa mahututi. Inaelezwa kuwa, maelfu ya watu walikuwa wamehudhuria katika ibada hiyo iliyomalizika majira ya usiku.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment