Thursday, 20 November 2014

MWAKYEMBE ASULUBIWA


Kambi ya upinzani Bungeni jana ilimsulubu Waziri wa Uchukuzi Dk.Harrison Mwakyembe ikieleza kuwa Wizara yake iliingia mkataba wa mradi wa treni za kisasa kutoka stesheni ya Dar es salaam hadi Pugu kupitia uwanja wa ndege wa JNIA bila kufuata taratibu.
Kambi hiyo ilieleza Bungeni kuwa mkataba huo ulisainiwa baina ya mmliliki wa kampuni ya M/S Shomoja Robert Shumake na Shirika la Reli Tanzania huku Waziri huyo akishuhudia live.
Msemaji mkuu wa kambi hiyo ya upinzani Pauline Gekul alisema taratibu hazikufuatwa  na kuwa haieleweki ni lini Serikali,Wakala au Wizara ya uchukuzi ilitangaza Zabuni ya mradi wa treni kutoka stesheni hadi pugu kupitia JNIA.
Alisema ni wazi kwa kifupi Mwakyembe na Wizara yake walikiuka vifungu vya sheria ya PPP na alivitaja vifungu hivyo kuwa ni  4(1) na(2) vinavyomtaka Waziri kutangaza katikaGazeti la Serikali miradi mbalimbali inayotegemewa kufanywa na sekta ya umma kwa ubia na sekta binafsi.       

No comments: