Wednesday, 19 November 2014
MISS HONDURUS AFARIKI SIKU 25 KABLA YA KWENDA MISS WORLD
Zikiwa zimebaki siku 25 kabla ya kufanyika kwa shindano la Miss World mwaka 2014 ,Miss Hondurus Maria Jose Alvaroe pamoja na dada yake Sofia Trinidad Alvaroe mwenye miaka 23 wamekutwa wamekufa baada ya kupotea kwa siku sita.
Kwa mujibu wa kituo cha BBC tukio hilo lilitokea alhamisi ya wiki iliyopita wakati wakisherehekea siku ya kuzaliwa ya rafiki wa dada yake ikiwa ni siku moja kabla mrembo huyo mwenye miaka19 hajaondoka kuelekea jijini London tayari kwa ajili ya kushiriki shindano hilo.
Polisi nchini humo wamesema mpaka sasa bado hawajafahamu chanzo cha mauaji hayo pamoja na wahusika na tukio hilo lakini mashuhuda wanasema wasichana hao waliondoka kwenye sherehe hiyo wakiwa na gari ndogo ambayo halikuwa limesajiliwa.
Taarifa za kupotea kwao zilipatikana jumapili baada ya kutorejea nyumbani huku simu zao zikiita bila majibu.
“Siku zinakwenda bila kuwaona wanangu,lazima polisi watakua na majibu ya haya”alisema mama mzazi wa wasichana hao.
Miili yao ilipatikana leo asubuhi katika eneo ambalo inasemekana walionekana kwa mara ya mwisho wakiwa wote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment