Thursday, 20 November 2014

COSBY ATUHUMIWA KUFANYA UDHALILISHAJI 1980'S


Televisheni ya NBC imesitisha mradi wa kurusha kipindi cha mchekeshaji maarufu duniani, Bill Cosby baada ya kukabiliwa na shutuma zaunyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake .

Katika taarifa hiyo, kampuni imethibitisha kusimamishwa kwa kipindi hicho.

Siku ya jumanne kamouni inayotoa huduma ya vipindi vya video kwa njia ya internet, Netflix iliahirisha kipindi kilichomuhusu Cosby baada ya mwanamitindo mmoja kudai kuwa alidhalilishwa kijinsia mwaka 1982.

Mtandao wa Netflix ulikataa kutoa sababu ya kusitisha uzalishaji wa kipindi, lakini umesema kuwa maandalizi ya uzalishaji ulikua haujaanza.

Cosby amekana kuhusika na vitendo hivyo.

Hatua hii imekuja baada ya mwanamitindo na mtangazaji kipindi cha Televisheni Janice Dickinson kusema kuwa alidhalilishwa na Cosby walipokutana kwa ajili ya chakula cha usiku huko California mwaka 1982.

Janice amesema aliandika katika kitabu kinachohusu maisha yake kuhusu tukio hilo lakini alipata shinikizo kutoka kwa Mwanasheria wa Cosby na mchapaji wa kitabu chake kuondoa sehemu hiyo.

Mwanasheria wa Cosby Martin Singer amesema madai ya Dickinson ni ya uongo na hayana msingi.

Dickinson ni miongoni mwa wanawake kadhaa waliomshutumu kuwadhalilisha kijinsia miaka takriban 30 iliyopita.

Nae muigizaji wa zamani Barbara Bowman amesema alidhalilishwa na Cosby katika nyakati tofauti mwaka 1985 alipokuwa na umri wa miaka 17.

Mwanzoni mwa mwezi huu Barbara alisema alishindwa kupeleka mashitaka polisi kwa kuwa alihofu hataaminika.

Cosby hajawahi kushtakiwa kwa kosa lolote la kihalifu.

No comments: