Thursday, 20 November 2014

AJIKATA UUME...KISA NA MKASA? SHUKA NAYO...!!!!


Jamaa mmoja EvgvinSapeev mwenye miaka 38 nchini Urusi  ametoa kali ya kufungia mwaka baada ya kujikata  kikojoleo almaarufu uume ilimradi ageuke kuwa mwanamke.
Kikubwa kilichomfanya jamaa huyo ambaye ni msanii wa filamu kujikata kiungo hicho muhimu cha uzazi ni kwamba alitamani siku moja kugeuka kuwa mwanamke kutokana na kuvutiwa na wanawake.
Mwanaume huyo alionekana akitoka nje ya nyumba yake huku damu zikimtoka mithili ya bomba la Dawàsco lililohàribika koki kutokana na kitendo hicho ambacho alikifanya mwenyewe na watu kuamua kumkimbiza hospitali baada ya hali yake kuwa mbaya.
Madaktari walijaribu kumshona ili kurejesha maumbile yake lakini hawakufanikiwa na alivuja damu nyingi ambazo zilihatarisha maisha yake kwani angeweza kufariki.
Baadhi ya majirani zake walimkosoa msanii huyo kujikata sehemu za siri badala ya kwenda hospitali kufanyiwa upasuaji kwa njia iliyo salama.....Majuu kweli hamnazo...!!!!

No comments: