Thursday, 20 November 2014
JULIO: SINA HAJA NA MSUVA NINALO JEMBE MROPE
“ Siwezi kumtafuta Msuva wakati nina Mrope anayecheza winga na mwenye kasi nzuri kama yake. Tena ana kasi kuliko Haruna Chanongo wa Simba.”
Baada ya kuvuma habari kuwa Simba imepanga kuifuata Yanga ili kumsajili winga wao machachari, Simon Msuva kocha mkongwe Julio amedai klabu yake isingeweza kumfuata winga huyo kipindi hiki kwani tayari ina kiboko yake.
Tayari, Mwadui inaye Julius Mrope, mchezaji ambaye Julio anaamini ana uwezo unaofanana na Msuva.
Alisema: “ Siwezi kumtafuta Msuva wakati nina Mrope anayecheza winga na mwenye kasi nzuri kama yake. Tena ana kasi kuliko Haruna Chanongo wa Simba.”
Mrope aliyewahi kutamba akiwa Yanga, Simba na baadaye Kagera Sugar ameanza kwenye michezo minane kati ya kumi iliyocheza Mwadui msimu huu kwenye Ligi Daraja la Kwanza.
“Unajua Mwadui inaweza kusajili mchezaji yoyote tunayemtaka, lakini mimi binafsi nataka kusajili na kuwatengeneza upya wachezaji ambao hawakuaminiwa na kuwarudisha kwenye viwango vya juu huku wakipata mafanikio,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment