Thursday, 20 November 2014
LUTENI KANALI ISAAC ZIDA ATEULIWA KUWA WAZIRI MKUU WA BURKINA FASO
Afisa wa cheo cha juu wa jeshi ambaye alikamata madaraka kwa muda mfupi nchini Burkina faso ametajwa waziri mkuu wa serikali ya mpito ya nchi hiyo.
Uteuzi wa Luteni Kanali Isaac Zida ulitangazwa Jana 19 November, siku moja baada ya rais wa muda Michel Kafando kuapishwa Jumanne mjini Ouagadougou.
Hakuna majibu kutoka Umoja wa Afrika, ambayo ilitishia vikwazo dhidi ya Burkina Faso mpaka Luteni Kanali Zida arejeshe madaraka kwa serikali inayoongozwa kiraia.
Jeshi limemtaja Luteni Kanali Zida mkuu wa nchi hapo Novemba mosi baada ya Rais wa muda mrefu Blaise Compaore kujiuzulu baada ya kukabiliwa na upinzani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment