Thursday, 20 November 2014

AVEVA: HATUNA NAFASI YA KUSAJILI WACHEZAJI WA KIGENI


Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva amesema kwamba hawana nafasi ya kusajili ya mshambuliaji wa kigeni na kwamba Emmanuel Okwi, Amisi Tambwe na Paul Kiongera wanawatosha.
Kauli hiyo ya Aveva inakuja wakati tayari vyombo vya habari vimekuwa vikiwahusisha washambuliaji Mnigeria, Emeh Izuchukwu na Mganda Danny
Sserunkuma kusajiliwa na Simba.
Aveva amesema kwamba Izuchukwu ambaye ni mchezaji wao wa zamani, ameomba mwenyewe kurejea kuchezea klabu hiyo, lakini anasikitika hawana nafasi ya mchezaji
wa kigeni.
“Hao wachezaji wengine hao, ni magazeti tu yamekuwa yakiandika, lakini ukweli ni kwamba hatujazungumza nao,”amesema Aveva

No comments: