Saturday, 22 November 2014

BAADA YA KUKATALIWA KUPANDA NDEGE KWENDA INDIA KWA MATIBABU,KIJANA WA KITANZANIA AFARIKI DUNIA


Sande Jacob Mremi (pichani) amefariki Siku chache baada ya kukosa usafiri wa ndege ambapo alitakiwa kwenda nje ya nchi kupata matibabu.
Kituo cha ITV kiliripoti kuhusu habari za kijana huyo kuumwa na kutokana na kusumbuliwa tatizo la uzito mkubwa nakushindwa kupata Ndege ya kumsafirisha kwenda kwenye matibabu India kijana huyo amefariki Dunia.
Ndugu wa kijana huyo walilalamika kutoridhishwa na baadhi ya Mashirika ya Ndege kwa kushindwa kuwasaidia kumsafirisha ndugu yao.
Katika mahojiano na ITV mama wa mtu huyo amesema; “..yaani kwa kweli mashirika ya Ndege hayakuweza kutufanyia haki kwa kweli, wametunyanyasa kwa sababu tulipokuwa tunapeleka maombi tunataka kumsafirisha mtoto wetu ilikuwa wao watusaidie na kutupa maelekezo tunatakiwa tufanye nini na nini, lakini baada ya kuona tunakosa msaada ndio tukaamua kuja ITV ili watusaidie, kwa hiyo yeye mwenyewe akaanza kupata presha kwa sababu presha alikuwa hana mpaka anapanga kusafiri alikuwa hana presha nilimpima vipimo vyote alikuwa hana tatizo lolote…”
Dada wa marehemu amesema; “..Ethiopia walitusaidia kwa kweli mpaka hatua ya mwisho na Jumapili kama Mungu angemuweka hai Ethiopia wangemsafirisha, na mashirika ya Ndege mengine yalitakiwa yatuelekeze hivi, lakini sasa kutokana na ile hali mara leo kapelekwa kesho anarudishwa mdogo wangu kesho kutwa kapelekwa amerudishwa mdogo wangu, msongo wa mawazo umemkaa rohoni anashindwa kuongea maskini ya Mungu, mawazo paka yamemfanya mdogo wangu alikuwa hana presha paka presha imekuja paka mdogo wangu anafariki.

Baba wa Sande amesema; “…wakatumia sheria ya pili ya kunihusisha mimi wakaniambia bwana kumbe mtu huyu ni mkubwa sana tunatakiwa tuvunje viti tumbebe, nikawauliza nikulipeni bei gani? wakaniambia tulipe dola elfu saba mia tano na thelathini na nne, na mara ya kwanza tulilipa dola elfu sita miambili ishirini…”
Bado haijafahamika kama Shirika hilo la ndege litarudisha hela ambayo ililipwa na watu hao kwa ajili ya kumsafirisha ndugu yao.

No comments: