Thursday, 20 November 2014
MKURUGENZI WA KAMPUNI ILIYOTENGENENZA FERRY ILIYOZAMA KOREA NAE AENDA JELA
Mahakama moja nchini Korea kusini imemhukumu miaka kumi gerezani mkurugenzi mkuu wa kampuni iliyoitengeza feri ya Sewol iliyozama mwezi Aprili na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 300, wengi wao wakiwa ni watoto.
Mahakama ya wilaya ya Gwangju imeelezwa kwamba feri hiyo ilikarabatiwa kuweza kubeba mizigo zaidi na mabadiliko hayo yaliongeza uwezekano wa chombo hicho kupindukia.
Mapema mwezi hu kapteni wa feri hiyo, alihukumiwa miaka 36 kwa kukwepa majukumu yake.
Mmiliki wa kampuni hiyo alifariki akitoroka.
Wapiga mbizi waliiokoa miili 295 kabla ya serikali kusitisha shughuli hiyo ya kutafuta miili zaidi wiki iliyopita. Bado waathirwa tisa hawajulikani waliko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment