Saturday, 22 November 2014

ARSENAL YAWAKOSA MESSI NA PIQUE


Kocha wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kuwa kilabu hiyo ilijaribu kumsajili nyota wa kilabu ya barcelona Lionel Messi kama mpango wa kutaka kuwanyakua wachezaji watatu wachanga wa kilabu hiyo.

Messi alikuwa na miaka 15 wakati huo na mwenzake Gerrad Pique pamoja na aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Cess fabregas.

Wenger:''Tulitaka kumchukua Fabregas,Messi na Pique,lakini tukafanikiwa kumpata Fabregas pekee''.

Fabregas aliichezea kilabu ya Arsenal kwa miaka minane kabla ya kurudi Barcelona ,huku Pique akijiunga na Manchester United mwaka 2004.


Messi mwenye umri wa miaka 27,ameichezea timu ya Barcelona kwa muda wote na kuisadia kushinda mataji sita ya La liga pamoja na kombe la vilabu bingwa mara tatu baada ya mpango wa kujiunga na Arsenal kugonga mwamba.

Hatahivyo ,Wenger amepinga madai kwamba mpango huo ulifeli kutokana na makaazi ya Messi na familia yake. Mchezaji huyo wa timu ya Argentina pia angelazimika kuwa na kibali cha kufanya kazi nchini Uingereza.

Wenger aliongezea:''Nadhani Messi mwenyewe hakutaka kujiunga nasi''.

No comments: