Thursday 20 November 2014

LUNDENGA: SITTI HARUDISHI ZAWADI HATA MOJA




Mkurugenzi wa LINO International Agency ambao ni waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga amesema miongoni mwa maswali aliyokutana nayo kwa wingi jana kwenye ‘Kikaangoni’ ya EATV, ni pamoja na swala la Sitti Mtemvu kama atanyang’anywa zawadi alizopewa ili akabidhiwe aliyevishwa taji hilo baada ya yeye kujivua.“Kwanza hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania mtu kujivua taji, na kwenye kanuni zetu haikuelezwa wazi wazi kwamba mtu akivua taji tunachukua zawadi tunamkabidhi mtu mwingine ama hivyo,” Lundenga ameiambia E-Newz ya EATV.   Lundenga amesema kuwa Sitti hatanyang’anywa zawadi kwasababu hakuvuliwa taji bali alijivua mwenyewe.

No comments: