Thursday, 20 November 2014

MAGAIDI 50 RAIA WA UFARANSA WAANGAMIZWA NCHINI SYRIA



Waziri mkuu wa Ufaransa amekiri kwamba vijana 50 wa nchi hiyo waliokuwa wakipigana bega kwa bega na makundi ya kigaidi na kitakfiri nchini Syria wameuawa nchini humo.

Manuel Valls amesema jana kuwa, karibu vijana elfu moja wa Kifaransa wamejiunga na makundi ya kigaidi na kitakfiri  nchini Syria kwa shabaha ya kupigana na serikali ya nchi hiyo. Waziri Mkuu wa Ufaransa amebainisha kuwa, takwimu hizo zitaipa changamoto kubwa serikali ya Paris katika kupambana na makundi ya kigaidi.

Matamshi ya Waziri Mkuu wa Ufaransa yanatolewa katika hali ambayo, Marine Le Pen kiongozi  wa chama cha Nation Front amesisitiza kuwa, hivi sasa kuna karibu  vijana elfu nne wa Kifaransa wanaopigana dhidi ya serikali ya Syria. Serikali ya Ufaransa pamoja na madola mengine ya Magharibi yalikuwa mstari wa mbele katika kuyaunga mkono kifedha na kisilaha makundi ya kigaidi na kitakfiri, lakini hivi sasa wanaonyesha eti kushangazwa  kwa raia wao kujiunga na makundi hayo ya kigaidi. Madola ya Magharibi yanahofia kushuhudia wimbi la mashambulio ya kigaidi kwenye nchi zao, pindi magaidi hao watakaporejea kwenye nchi zao katika siku za usoni.   

No comments: