Thursday, 20 November 2014

MSD YAANZA KUSAMBAZA MADAWA NCHI NZIMA


Bohari kuu ya Dawa MSD imeanza kusambaza dawa katika hospotali mbalimbali nchini ba ada ya kupokea kiasi cha bilioni20 ambazo ni sehemu ya malipo ya deni linaloidai Serikali
Kaimu Mkurugenzi mkuu wa MSD Cosmas Mwaifani alisema fedha hizo zitapunguza kwa kiasi kidogo cha deni hilo ingawa alisema bohari hiyo haijawahi kukataa kutoa dawa katika hospitali.
“Kama wana fedha za kutosha hilo kwetu si tatizo kwa sababu dawa tunazo,wakifuata masharti ya ununuzi sisi tunawapa dawa”alisema.
Alisema fedha walizopewa tayari zimeshaingizwa katika mzunguko wa ununuzi wa dawa kwa baadhi ya hospitali kwa kufuata vipaumbele na kuhusu shehena ya dawa kukwama bandarini ni kawaida kwa mizigo kukwama kutokana na mchakato mrefu wa utoaji mizigo ambao unahusisha sehemu nyingi za ukaguzi na uthibiti.
Kauli ya Mwaifani imekuja wakati kukiwa na taarifa kutoka hospitali mbalimbali hasa za Serikali  ambao watendaji wake wakuu wamedai kwamba hawajapokea dawa toka MSD badala yake wametumia njia mbadala ikiwa ni pamoja na kutumia fedha wanazokusanya kutoka kwa wagonjwa kwa ajili ya kununulia dawa za wa dharura.

No comments: