Thursday, 20 November 2014
MAZUNGUMZO YA NYUKLIA YA IRAN,5+1 YAENDELEA VIENNA
Wawakilishii wa Iran na kundi la 5+1 wanaendeleza mazungumzo ya nyuklia katika mji mkuu wa Austria, Vienna kwa lengo la kufikia mapatano ya muda mrefu kuhusu miradi ya nyuklia ya Iran.
Wanadiplomasia wa Iran na wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa yaani China, Russia, Ufaransa, Uingereza na Marekani pamoja na Ujerumani leo wameendelea na mazungumzo kwa siku ya pili kama sehemu ya duru ya mwisho ya mazungumzo ya kufikia mapatano kabla ya muhula uliowekwa wa Novemba 24.
Juzi mjini Vienna Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Jahad Zarif alifanya mazungumzo na Catherine Asthon, mwakilishi mkuu wa madola sita makubwa duniani katika mazungmzo ya nyuklia. Duru zinasema, ajenda kuu ya mazungumzo hayo ni kuondolewa vikwazo dhidi ya Iran. Imearifiwa kuwa Iran inataka vikwazo viondolewa kikamilifu lakini Marekani, chini ya mashinikizo ya utawala haramu wa Israel, inataka vikwazo, haswa vilivyowekwa na Umoja wa Mataifa, viendelee kuwepo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment