Thursday, 20 November 2014
FIRST ELEVEN MPYA YA SIMBA SC HII HAPA.....hatoki mtu round ya pili..
Matokeo yasiyoridhisha ya Simba katika Ligi Kuu msimu huu yameufanya uongozi wa klabu hiyo uchanganyikiwe na kutaka kusajili kila mchezaji wamwonaye wakati huu wa usajili wa dirisha dogo.
Kutokana na presha hiyo, uongozi wa klabu hiyo umeshataja orodha ya wachezaji 11 ambao inataka kuwasajili kwa sasa ili kuimarisha kikosi.
Uongozi wa klabu hiyo unaonekana kuwataka wachezaji wengi kuliko timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu na baadhi ya timu zimeonekana hazina mpango wa kuongeza wachezaji, nyingine zikitaka kuongeza wachache.
Alipoulizwa kuhusu usajili huo, katibu mkuu wa Simba, Stephen Ally alijibu:
“Kwanza, nani alisema tunawasajili wachezaji hao, hizo ni stori za vijiweni na za magazetini hivyo siwezi ku-comment (kusema lolote). “
Hata hivyo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa hadi sasa Simba imetangaza kuwataka wachezaji 11, idadi ambayo ni sawa na kikosi kizima cha kwanza.
Wachezaji wanaohusishwa na usajili mpya Simba ni kipa Juma Kaseja (Yanga), Said Morad (Azam), Emeh Izuchukwu (Elverum Fc, Norway), Danny Mrwanda (Polisi Moro), Dan Sserunkuma (Gor Mahia, Kenya), Hamis Kessy, Salim Mbonde, Ame Ally (Mtibwa Sugar), Deus Kaseke (Mbeya City), Nurdin Chona na Salum Kimenya wa Prisons.
Kwa maana hiyo, Simba inaweza kucheza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu kwa ufasaha ikiwa na wachezaji wapya zaidi ya waliocheza mechi saba na waliokuwapo huenda wakaishia benchi.
Kulingana na wachezaji hao kikosi cha kwanza Simba kinaweza kuwa:
Juma Kaseja, Salum Kimenya, Hamis Kessy, Said Morad, Salim Mbonde, Nurdin Chona, Dan Sserunkuma, Deus Kaseke, Ame Ally, Danny Mrwanda, Emeh Izuchukwu. Hata hivyo kuna baadhi ya wachezaji itakuwa vigumu kwa Simba kuwanasa msimu huu.
Miongoni mwao ni Izuchukwu, raia wa Nigeria anayesemekana anapigiwa chapuo na kigogo mmoja wa timu hiyo, lakini baadhi ya viongozi hawakubalini na hilo.
Beki Morad anatakiwa abadilishane na kiungo Amri Kiemba kwenda Azam, ndipo aachiwe atue Msimbazi.(MWANANÇHI)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment