Wednesday, 19 November 2014
MENO YA TEMBO YAIBWA MIKONONI MWA SERIKALI
Maafisa Wanyamapori watano wamesimamishwa kazi ili kupisha upelelezi kufanyika kufuatia kupotea kwa meno ya tembo kwenye mazingira ya kutatanisha yakiwa katika sehemu ya ulinzi mkali wa Serikali, Uganda.
Akizungumza na AFP mkurugenzi wa Uganda Wildlife Authority, Raymond Engena amesema wameomba msaada wa Kikosi cha Askari wa Kimataifa (Interpol) kufanya upelelezi kufuatia agizo la Rais Museveni la kutaka wahusika wote kukamatwa kutokana na upotevu huo.
Meno hayo yana uzito wa kilo 1,335 yana thamani ya Dola Mil. 1.1 za Uganda ambapo imesemekana baadhi ya maofisa hao wamekuwa wakiyachukua meno hayo kwa ajili ya kutumia kuwatega wafanyabiashara wa meno hayo lakini hawayarudishi baada ya kuyafanyia kazi hiyo.
Ripoti zinaonyesha idadi ya tembo 35,000 wamekuwa wakiuawa Afrika kila mwaka kutokana na biashara hiyo kuonekana kuwa na soko kubwa nchi za Asia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment