Thursday, 22 January 2015
MASIKINI TAMBWE ASIMULIA ANAVYONYANYASIKA,YANGA YAKIMBILIA TFF KUSHTAKI
Klabu ya Yanga imepanga leo kuwasilisha malalamiko yao juu ya tukio la kunyanyaswa kwa mshambuliaji wake Amissi Tambwe kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lakini pia mchezaji husika amefafanua kwa kina juu ya manyanyaso anayoyapata.
Akizungumza mchana huu katika makao makuu wa klabu hiyo Mkuu wa Kitengo cha Habari Jerry Muro amesema uongozi wao unakusudia kuwasilisha malalamiko yao hayo ambayo mengi yametokana na vitendo alivyofanyiwa Tambwe wikiendi iliyopita katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambapo wanataka mapendekezo yao manne yafanyiwe kazi.
Muro amesema kwanza Yanga ingwetaka kuona TFF inawachukulia hatua kali wahusika wote waliomdhalilisha Tambwe huku pili wakilitaka shirikisho hilo kutoa hadharani taarifa ya tathimini ya waamuzi wa mchezo huo lengo likiwa ni kujua
umakini wa waamuzi hao.
“Tatu tungewaomba wenzetu wa TFF kwa kuwa wao wapo kimya pia kuwachukulia hatua wahusika wote waliosimamia mchezo huo kwa kushindwa kubaini haya ambayo vyombo vya habari imeyafichua lakini ikiwezekana wafungiwe na Yanga hatuwataki kuwaona wanachezesha mechi zetu vinginevyo tutagoma na hata Ruvu nao tungependa kuona wanapewa adhabu kwa viongozi wao kushabikia maovu haya.
Aidha Tambwe mwenyewe amechukizwa na matukio hayo akisema ameshangazwa kuona anafanyiwa vitendo vya kinyama ambapo mengine hawezi kuyaweka hadharani.
“Mpira ni starehe mimi sikatai mchezaji anikabe lakini ni jinsi gani unanikaba hapo ndiyo tatizo, naambiwa mimi mkimbizi hivi hawa wenzangu wanajua maana na haya maneno yapo mengi ambayo nimedhalilishwa nayo kiungwana siwezi kuyaweka wazi hapa lakini viongozi nitawaeleza,”alisema Tambwe.CHANZO SHAFIH DAUDA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment