Wakati suala la ajira likiwa bado ni kitendawili kikubwa kwa serikali, Jiji la Dar hivi sasa linatisha, baada ya watu kubuni mtindo mpya wa kujipatia fedha kwa kujihusisha na biashara haramu ya ngono katika maeneo yanayotambulika kufanya shughuli nyingine halali.
Uchunguzi unaonyesha kuwa zipo saluni nyingi jijini Dar zinazojishughulisha na biashara ya massage (kuchua) lakini ndani yake wahudumu wanajiuza hadi miili ambapo wateja wakubwa ni waume za watu na vigogo serikalini.
Uchunguzi huo unathibitishwa na tukio moja la hivi karibuni lililonaswa na polisi katika saluni moja ya kuchua iliyopo eneo la Kinondoni-Morocco, Dar. Polisi hao walikuwa katika msako baada ya kudokezwa maovu yanafanyika ndani ya saluni hiyo.
Ndani ya saluni hiyo, Polisi walishuhudia mhudumu wa mapokezi ambaye baada ya kuonyeshwa vitambulisho vya askari wa Jeshi la Polisi, alinywea na kuwaruhusu kupekua chumba kimoja baada ya kingine, ili kujionea kama kweli nyumba hiyo ilikuwa ikijihusisha na masuala ya saluni ya uchuaji pekee na siyo vinginevyo.
Katika chumba cha kwanza, askari hao walimkuta mwanaume mmoja akiwa uchi wa nyama, lakini mwanamke aliyekuwa naye akiwa amevaa nguo zake, kitu kilichoashiria kuwa tayari ‘mchezo ulishafanyika’.
Katika hali isiyotarajiwa, baada ya kupitia vyumba vingine vinne na kuvikuta tupu, kilichofuata, polisi walishuhudia mwanamke mwenye asili ya Kisomali akiwa uchi na mwanaume wake, dalili zote zikionyesha kuwa walikuwa wakijiandaa kufanya uzinzi.
Baada ya kuwakuta katika hali hiyo, kiongozi wa askari hao, aliwauliza kama hiyo ndiyo biashara ya masaji waliyopata kibali cha kuifanya, lakini wakabakia kujiumauma pasipo kutoa jibu la kueleweka.
Binti huyo wa Kisomali, ghafla aliibuka na kuanza kuomba msamaha kwa kitendo hicho, akidai maisha magumu wanayoishi, ndiyo yanayosababisha waifanye biashara hiyo.
Lakini la kushangaza zaidi, ni pale mwanamke huyo alipodai kuwa nyumbani alikotoka, ambako ameolewa, pia alimuacha mwanaye mwenye umri wa miezi minne.
Mwanaume aliyekutwa naye, alipoulizwa biashara hiyo inafanyika kwa bei gani, alisema makubaliano yake na mwanamke huyo, ni kutoa kiasi cha shilingi elfu sitini kwa tendo moja!
No comments:
Post a Comment