Friday, 12 December 2014
YANGA YAMTEMA KHAMIS KIIZA
Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika , klabu ya Yanga ipo mbioni kukatisha mkataba na mshambuliaji Hamis Kiiza raia wa Uganda,
‘’Tutakaa chini kuzungumza na Kiiza ili kuangalia namna ya kuachana kwa amani,baada ya Mliberia kufuzu vipimo vya afya hatuna jinsi lazima tuliondoe jina la Kiiza kwenye usajili wetu,kilisema chanzo hicho ‘’
Yanga inalazimika kupunguza mchezaji mmoja wa kigeni hasa baada ya mshambuliaji Kpah Sean Sherman kufuzu vipimo vya afya na kuwa mbioni kusaini mkataba na klabu hiyo,
Hivi karibuni Yanga ilimsainisha kiungo Emerson toka nchini Brazil mkataba wa mwaka mmoja,ukiachana na Kiiza wachezaji wengine wa kigeni ndani ya klabu ya Yanga ni Mbuyu Twite,Haruna Niyonzima, Kpah Sean Sherman na wabrazil Courtinho na Emerson.
Ikumbukwe Idadi ya wachezaji wa kigeni wanaotakiwa kusajiliwa na timu ni watano.
CHANZO SHAFFI DAUDA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment