Tuesday, 9 December 2014
WALE MAPACHA WALIOUNGANA HUKO INDIA WAPATA MPENZI..
Mapacha ambao wameungana huko Bengal Magharibi Ganga na Jamuna Mondal 45, wamesema hawajawahi kuwa na mpenzi katika maisha yao kwa sababu ya kukataliwa kutokana na mwonekano wao.
Mabinti hao ambao wanatumia mikono minne na miguu mitatu wamesema kwa sasa wanafuraha ambayo hawajawahi kuwa nayo katika maisha yao baada ya kukutana na mwanaume aliyewapenda kwa mara ya kwanza Mwalimu Jasimuddin Ahmad.
“… Wakati tunakutana na Jasimuddin wote tuliona kuwa huyu ni mwanaume ambaye ana upendo wa kweli kwetu, ni kweli anao… anatupenda kweli toka moyoni mwake, tuna furaha toka aje maishani mwetu.. tuliteseka huko nyuma lakini hatutaki kuteseka tena, kwa kweli tuna matumaini ya kuwa naye muda wote wa maisha yetu”, wamesema mapacha hao.
Mabinti hao ambao wanatumia Tumbo moja walizaliwa kwenye familia masikini karibu na Kolkata, Magharibi mwa Bengali, wazazi wao walishindwa kumudu gharama za kuwatenganisha maungo yao walipokuwa wadogo.
Waliwahi kujiunga na kampuni ya kucheza Sarakasi ambapo walikuwa wakisafiri kwa kufanya maonyesho mbalimbali huko India ambapo ndipo walikokutana na Ahmed.
“Tangu nikutane nao nilichukulia maumivu yao kama ya kwangu mwenyewe daima nitakuwa hivi, nimekuwa nikitibu matatizo ya watu wengine kama yangu na kujaribu kufanya mambo mazuri” alisema Ahmed.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment