Tuesday 9 December 2014

MAUAJI YAENDELEA JIJINI MBEYA


MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA NTOKELA WILAYANI RUNGWE ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA CHESCO MAHENGE (41) ALIKUTWA AKIWA AMEUAWA KWA KUCHOMWA NA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI NA WATU WASIOFAHAMIKA.MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA KANDO YA BARABARA KWENYE MASHAMBA YA CHAI MNAMO TAREHE 07.12.2014 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MAPINDUZI, KIJIJI CHA NTOKELA, KATA YA ISONGOLE, TARAFA YA UKUKWE, WILAYA YA RUNGWE, MKOA WA MBEYA.


MWILI WA MAREHEMU ULIKUTWA UKIWA NA MICHUBUKO SEHEMU ZA MGONGONI.INADAIWA KUWA MNAMO TAREHE 06.12.2014 MAJIRA YA SAA 17:00 JIONI MAREHEMU ALIONDOKA NYUMBANI KWAKE AKIAGA KUWA ANAKWENDA MATEMBEZI KIJIJINI HAPO. CHANZO CHA MAUAJI KINACHUNGUZWA INGAWA UCHUNGUZI WA AWALI UNAONYESHA MAREHEMU ALIKUWA ANATUHUMIWA KWA TABIA YA WIZI KIJIJINI HAPO SIKU ZA NYUMA.KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO. AIDHA ANATOA WITO KWA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA BADALA YAKE WAWAFIKISHE WATUHUMIWA WANAOWAKAMATA KWA TUHUMA MBALIMBALI KATIKA VYOMBO VYA SHERIA KWA HATUA ZAIDI ZA KISHERIA.

KATIKA TUKIO LA PILI:
MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA NDAGA WILAYANI RUNGWE ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA ZELII MWAITAVILA (70) ALIFARIKI DUNIA AKIWA ANAJIUGUZA NYUMBANI KWAKE ANAPOISHI PEKE YAKE BAADA YA KUSHAMBULIWA NA WATU WASIOFAHAMIKA.
MAREHEMU ALISHAMBULIWA KWA KUPIGWA MNAMO TAREHE 27.11.2014 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI NYUMBANI KWA HAMIS MATEO NA KURIPOTI KITUO CHA POLISI NA KUFUNGUA KESI KISHA KUPEWA PF.3. HATA HIVYO HAKURUDI TENA POLISI HADI ZILIPOPATIKANA TAARIFA ZA KIFO CHAKE.
WATUHUMIWA WAWILI AMBAO NI 1. HAMISI MATEO (41) NA 2. SAMWEL SAMSON MWANAWAMBUGA (47) WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA NDAGA WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA KATIKA TUKIO HILO. CHANZO CHA TUKIO HILO NI IMANI ZA KISHIRIKINA BAADA YA WATUHUMIWA KUMTUHUMU MAREHEMU KUWA NI MCHAWI.
TAARIFA ZA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA MKAZI WA KIJIJI CHA LUALAJE WILAYANI CHUNYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA MASUNGA LUSEBELO (23) AKIWA NA POMBE YA MOSHI UJAZO WA LITA 03.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 07.12.2014 MAJIRA YA SAA 13:50 MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA SUMBWE, KIJIJI NA KATA YA LUALAJE, TARAFA YA KIPEMBAWE, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA BAADA YA KUFANYIKA MSAKO KATIKA MAENEO HAYO. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA POMBE HIYO, TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

No comments: