Monday, 8 December 2014

DIAMOND AFANYA MAMBO YA AJABU SHEREHE ZA UHURU MAREKANI





Anaitwa rais wa Wasafi Diamond Platnumz akiwa pamoja na wacheza showa wake Roma Tonsa na Moses Iyobo wakitoa burudani ya nguvu katika sherehe ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania Bara iliyofanyika Sheraton Hotel ya Silver Spring, Maryland nchini Marekani na kuhudhuriwa na mashabiki wake kutoka kila pembe ya Marekani huku mashabiki wengine wakitokea Tanzania....

 
Unaambiwa ilikuwa ni Bonge moja ya shoo iliyowaacha watanzania hao waishio kwa Obama vinywa wazi huku wakitamani burudani iendelee mpaka majogoo...Makamuzi hayo ya nguvu toka kwa mtoto wa Tandale anayeing'arisha vema Tanzania worldwide yalimfanya spate pongezi maalum toka kwa balozi wa Tanzania aliye nchini humo...
Cheki picha zaidi hapa chini namna watu walivyokuwa wakiserebuka na vitorondo vya ajabu....

Balozi akimshukuru Diamond kwa kuwezesha kunogesha usiku wa Uhuru wa Tanzania na pia aliwashukuru wadhamini wa sherehe hiyo ya miaka 53 ya Uhuru wa Tanzania bara.



Kweli huyu Rais wa wasafi hebu cheki alivyopendeza .......

Cheki jinsi watu walivyokuwa nyomi....

Nadhani hapo kitorondo ndo kilikuwa kinapigwa.....Halafu cheki madola hayo yalivyomwagwa hapo chini......



Picha kwa hisani ya Vijimambo blog..


No comments: