Tuesday 9 December 2014

FEZA KESSY AMPIGA KIBUTI ONEAL..MWENYEWEEEE KAFUNGUKA



Mpenzi 
msomaji tunasikitika kukujuza kwamba ile ndoa iliyosubiriwa kwa hamu kubwa imeyeyuka baada ya uchumba wa staa wa Bongo Fleva aliyeiwakilisha Bongo kwenye Shindano la Big Brother Africa 2013 ‘The Chase’, Feza Kessy na jamaa kutoka Botswana, Oneal umeanguka chali.Habari za uhakika zinadai kwamba mwanadada huyo ndiye aliyeamua kukata mzizi wa fitina na kuachana na mwanaume huyo ambaye alitimba Bongo kumchumbia baada kuona hana mipango ya maisha ya baadaye huku jamaa akiwa bize na maisha yake na mwanaye mwenye umri wa miaka nane. 


                                               Feza Kessy akipozi.
Akizungumzia ishu hiyo, Feza alisema: “Mimi ndiye niliyemuacha. Nilitangaza kupitia Twitter (mtandao) lakini ujumbe umefika. Ni kweli tumeachana lakini siwezi kuzungumza in details (kiundani). Vitu vingine vitafunguka baadaye.

No comments: