Saturday, 13 December 2014

WAENDESHA BODABODA WA DAR WAMPA RAIS KIKWETE SIKU 14 TU LA SIVYO .............




Umoja wa waendesha Bodaboda na Bajaj Dar es Salaam wamesema wanampa Rais Kikwete siku 14 kushughulikia maombi yao ya kuruhusiwa kusafirisha abiria katikati ya Jiji kinyume na hapo wataitisha maandamano ya amani kushinikiza ombi lao kutekelezwa.

Mwenyekiti wa Chama hicho Said Chenja amesema hawaridhishwi na namna ambayo watendaji wa chini wa Rais wanavyoshughulikia suala hilo.
Mwenyekiti huyo amesema suala la utoaji wa vibali maalum limekuwa likifanywa kwa upendeleo mkubwa huku vibali hivyo vikiwa na mapungufu ya kutokuwa na maelekezo ya maeneo ambayo wale waliopewa vibali hivyo wanaruhusiwa kuingia na ambako hawaruhusiwi.

No comments: